×
Home: Mobile Home: Original Style What's New MP3 Bible Jewish Stories X-Witch X-Muslim Bible Movies Gospel Videos Godly Movies CBN Videos Random Video
  Kat Kerr   Anna Rountree   Mary Baxter   Several #1   Several #2   Choo Thomas   Ian McCormack   Burpo   I saw His Glory   7 Colombian Youths   Heavenly Blood   Heaven Testimonies
  Lazarus   Bill Wiese   Mary Baxter   Dr. Rawlings   J. Perez   Hepzibah   Ptr. Park   7 Columbian Youths
  Atomic Prayer   Prayers that ROUT demons   Warfare + Blessing   Healing   Declaration   101 Decrees   Tongues   Rosary   Artic Fire   Why Should We Pray?   Why Bother
  MP3 Bible   10 Commandments   Learn Bible in 24 Hours   40 Spiritual Lessons   Alpha   Foundations   Bible Commentaries   Book of Mormon   Temple Study   Red Letters   Divine Healing Training   God Story   Gap Theory   Creation to Christ   Book of John   Kids Bible Cartoons   Derek Prince Teaching   Jesus Film   Digital Bible   Bible Codes ELS
  Passion of Christ   New Jesus Film   Introduction   Names of God   Jesus IS...   Jesus Film   That's My KING   Father's Love Letter   Celestial Hug
  Warfare Training 1   Warfare Training 2   Casting Out demons   Combat   Examples   Warrior King   Exorcism   Prayer   Ask Him   demonology   Clarita   NUWI
  Final Quest   The Call   Tommy Hicks   3 Days   Angel Song   The Prison   H.A.Baker
  Best #1   Best #2   Spiritual Food   Generals   Ramirez   Bishop Kelley   Gary Wood   Roland Buck   Rees Howells   Baptized by Fire   Sid Roth   Todd White   Gary Beaton   Victor Marx   Akiane   Theo Nez   Nun's Story   Retha McPherson   Tomas Welch
  Booth's Vision   Frank Jenner   Hell's Best Kept Secret   EE-Taow   Manifesting Power   LivingWaters   Atheist Delusion   Using AI for Jesus   Sharing w/ Muslims   Sword + Serpent
  Revival Hymn   Jesus in China   Freemason Curruption   Modern Child Sacrifice   the WAR on Children   XGay   Transformations   Ark of Covenant   Soul Ties   Last Reformation   Noah's Ark Found   Does GOD Exist   Political Issues   Fake Mountain   7 Mountains   ID vs Evolution   Bible Science   American History   China Records   Case: Creator   Case: Christ   Case: Faith   Little Lessons   Deadly Mistakes   Enemies Within   Chinese Characters   Global Warming   The Final Frontier   Understanding Israel   Testing Joseph Smith   Targeting Kids
  X-Muslim   Journey of Hope   Islam Rising   ACT   Jihad   Best Muslim Story   Enemies Within   Answering Islam   Killing for Heaven   Killing the Infidel
  Downloadable MP3 Worship Music   Online Worship Music  DivineRevelations University   Free Posters   Christian Pictures   Kids Christian Cartoons   Bible Trivia   End Times Visions   Fractal Praise   Communion Verses   Bobby Conner   Brother Yun   Civil War   Prayer Tank   Fiscal Cliff   Understanding Economics   Who takes the Son   Christian GPTs
  All Languages   Afrikaans   Albanian   Amharic   Arabic   Bengali   Bulgarian   Burmese   Cambodian   Catalan   Chinese   Czech   Danish   Dutch   Farsi   Finnish   French   German   Greek   Gujarati   Hausa   Heberw   Hindi   Hungarian   Indonesian   Italian   Japan   Kannada   Khazanah   Korean   Laos   Malagasy   Malayalam   Malaysian   Marathi   Mongolian   Nepali   Norwegian   Oriya   Polish   Portuguese   Punjabi   Romanian   Russian   Somali   Samoan   Serbo_Croatian   Sinhala   Slovak   Slovenian   Spanish   Swahili   Swedish   Tagalog   Tamil   Telugu   Thai   Tongan   Turkish   Ukrainian   Urdu   Uzbek   Vietnamese
 About  Disclaimer  Phone# USA 425-610-9216  [email protected]
Follow on YOUTUBE  YouTube Follow on Facebook  Facebook Follow on X/Twitter  X/Twitter Follow Podcast RSS  Podcast  RSS Follow on Instagram  Instagram Follow on TikTok  TikTok
  PDF Library   Believer's Authority   Heavenly Man, Yun   Torch + Sword   The Harvest   Faith Shoemaker's Vision   Daughter of Sacrifice
For New Believers Something Funny... 2nd Page, Older Material
×






Menu / Home
Menu / Home


HTML Bible Passion of the Christ Gospel Go Ethnic Harvest Christian Video Gospel Tracks 4 Spiritual Laws MP3 Gospel of John HTML Bible CHM Bible (Windows Help Format) Translators Needed!


Swahili-Cango           Swahili Kenya           Swahili-Tanzania           Kuzimu na Kurudi           Ufunuo wa Yesu Kuhusu Kuzimu           MBINGUNI NA JEHANAMU: ELFU KWA MOJA           Dakika 23 Kuzimu na Bill Wiese           Masaa 8 Mbinguni           Kuzimu ni Halisi, nilikwenda huko!           Nafasi ya Pili--Ufufuo wa Theo Nez           Muujiza wa Uponyaji na Mualiko wa Mbinguni           Maono ya Unity           KWA NINI TUOMBE           Ufunuo wa Mbinguni           KUKOMBOLEWA KUTOKA KWENYE NGUVU ZA GIZA           Ufunuo wa Kuzimu

The Way to JesusUfunuo wa Mbinguni na Kuzimu wa vijana 7

Kwa pamoja kama kundi,vijana hawa 7 wa Kikolombia walichukuliwa na Yesu Kristo na walionyeshwa Mbinguni na Kuzimu.Sikiliza maneno yenye utukufu wa Mbinguni na Ubaya wa Kuzimu.
Translation help by Peter John Mlay
Kutokana na kumbukumbu tumeweza kuandika shuhuda 6 tu, zilizo tafsiriwa kutoka kanda ya kihispania,Picha ziliongezwa baadaye na hazikuwa sehemu ya ushuhuda. 

  -Heaven-
English  Spanish  Chinese
German  Dutch  Portuguese  Romanian
Korean  Swahili  French   Japanese
Swedish  Indonesian  Finnish  URDU
Afrikaans  Tagalog  Arabic  Italian Malagasy
Hausa  Hungarian  Thai  Malaysian

[www.minluznaciones.org]

--Hell--
English  Spanish 
German  Dutch
Korean Chinese/Trad  Russian Malagasy
Swedish  Swahili  Japanese  Bahasa Malaysian  Indonesian  Tagalog Amharic
Thai  Hungarian  Italian  Bulgarian
Arabic French   Finnish  Romanian
Portuguese  Tagalog   Hausa  URDU

Ufunuo wa Mbinguni
PDF   DOC   Ufunuo wa Kuzimu

--- (Ushuhuda wa kwanza, Esau) ---
2 Wakorinto 12:2 :
Namjua mtu mmoja katika Kristo,yapata sasa miaka kumi na minne-kwamba alikuwa katika mwili sijui;kwamba alikuwa nje ya mwili sijui;Mungu anajua-mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.
HeavenTulikuwa ndani ya chumba,wakati tulipo pata uzoefu huu wa kwanza.Chumba kilianza tena kujaa na utukufu wa Bwana.  Ulikuwa na nguvu sana kiasi kwamba ulikiangazia chumba chote.  Chumba kilikuwa kimejaa utukufu wake,ilikuwa ni jambo zuri kuwepo mbele zake. 
Yesu alituambia, "Watoto wangu wakiume,sasa nitawaonyesaho Ufalme wangu, tutakwenda kwenye utukufu wangu."  Tulishikana mikono na tuliinuliwa juu.  Nili angalia chini na niligundua kuwa tulikuwa tunatoka  nje ya miili yetu.  Tulipotoka nje ya miili yetu tulikuwa tumevaa mavazi meupe na tulianza kwenda juu kwa mwendo wa kasi sana.Tulifika mbele ya malango yaliyo fuatana ambayo ni njia ya kuingilia kwenye ufalme wa Mbinguni. Tulishangaa kile kilicho kuwa kina tutokea.   Shukrani nyingi,Yesu mwana wa Mungu alikuwepo pale pamoja nasi, pamoja na malaika wawili ambao kila mmoja alikuwa na mabawa manne.
Malaika walianza kuongea nasisi, lakini hatukuelewa kile walicho kuwa wanasema .  Lugha yao ilikuwa tofauti sana na ile ya kwetu, haikufanana na lugha yeyote ile ya duniani.  Malaika hawa walikuwa wakitukaribisha na waliifungua milango ile mikubwa sana. Tuliona eneo la ajabu sana, lenye vitu vingi tofauti tofauti. Tulipoingia ndani, amani ya kweli ilijaza miyoyo yetu.  Bibilia inatuambia kuwa Mungu atatupa amani ipitayo fahamu za kibinadamu (Wafilipi 4:7)
Kitu cha kwamza kukiona ilikuwa ni swala,hivyo nilimuuliza mmoja wapo wa marafiki zangu, "Sandra, je unaangalia kitu kile kile ninacho kiangalia?"  hakuwa analia  wala kupiga makelele tena, kama wakati ule tulipo onyeshwa kuzimu.  Alikuwa akitabasamu na alisema: "Ndiyo Esau, ninamwaangalia Swala!" Hivyo nilijua kuwa kila kitu kilikuwa halisi, kweli tulikuwa kwenye Ufalme wa Mbinguni. Hofu zote ambazo tuliziona kule Kuzimu haraka zilikuwa zimesahaulika. Tulikuwa mahali pale tukiufurahia utukufu wa Mungu. Tulikwenda mahali pale ambapo Swala yule alikuwepo, nyuma yake ulisimama mti mkubwa sana! Ilikuwa ni katikati ya bustani.

Bibilia inatuambia katika Ufunuo 2:7 "Yeye aliye na sikio,  na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.Yeyey ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu"

Mti huu ni ishara ya Yesu, kwasababu Yesu ni uzima wa milele.  Nyuma ya ule mti kulikuwa na mto wenye maji angavu.  Ulikuwa mweupe na mzuri sana, hatukwa tumewahi kuona tena kitu kama hiki duniani. Tulitaka tuu kubaki mahali pale. Mara nyingi tulimwambia Bwana, "Bwana tafadhali!  Usitutoe mahali hapa!  Tunataka kuwepo hapa milele!  Hatutaki kurudi tena duniani    Bwana alitujibu "Ni muhimu kwamba mrudi mkatoe ushuhuda wa kila kitu ambacho nimekiandaa kwa wote wale wanao nipenda, kwa sababu ninarudi mapema sana na ujira wangu u pamoja nami"
Tulipo ona mto, tulifanya haraka na tukaingia ndani yake.  Tulikumbuka msitari ule unao sema;Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena,mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.. (Yohana 7:38) Maji ndani ya mto huu yanaonekana yana uzima yenyewe, hivyo tulijizamisha wenyewe ndani yake. Ndani na nje ya yale maji tuliweza kupumua kawaida.  Mto ule ulikuwa na kina kirefu sana na kulikuwa na samaki wa rangi tofauti wakiogelea ndani yake.  Mwangaza ndani na nje ya maji ulikuwa wa kawaida; Mbinguni , mwanga hautoki kwenye kitu fulani,kila kitu kimetiwa mwangaza wake.  Bibilia inatuambia kuwa Bwana Yesu  (Ufunuo 21:23).  Kwa mikono yetu, tulichukua baadhi ya samaki, nje ya maji, hawakufa.  Hivyo tulimkimbilia Bwana na kumuuliza kwanini?  Bwana alitabasamu na alijibu kwamba Mbinguni hakuna tena kifo, hakuna kilio tena, hakuna maumivu tena (Ufunuo 21:4)

Tuli uacha ule mto na tulikimbia kila mahali tulipo weza, tulitaka kugusa na kuwa na uzoefu wa kila kitu.  Tulitaka kurudi na kila kitu nyumbani kwa ababu tulishangazwa sana na vitu vya mbinguni. Kwa kifupi huwezi kuvielezea kwa maneno.  Wakati Mtume Paulo alipochukuliwa  Mbinguni, aliona vitu ambavyo hakuweza kuvielezea kwa maneno, kwa sababu ya ukuu wa vitu vya Ufalme wa Mbinguni. (2 Wakorinto 12)  Kuna vitu ambavyo tuliviona ambavyo hatuna jinsi ya kuvielezea.
Baadaye tulifika kwenye eneo kubwa sana; eneo la ajabu na zuri sana.  Eneo hili lilikuwa limejaa mawe ya dhamani sana: dhahabu, emiradi, rubi na almasi.  Sakafu ilikuwa imetengenezwa na dhahabu halisi. Baadaye tulikwenda hadi eneo lenye vitabu vikubwa vitatu.  Cha kwanza kabisa kilikuwa ni Bibilia ya dhahabu.  Katika Zaburi inatuambia kwamba neno la Bwana linasimama imara mbinguni hata milele. (Zaburi 119:89) Tulikuwa tukiangalia Bibilia kubwa ya dhahabu; kurasa, maandiko, kila kitu kilifanywa kwa dhahabu halisi. 

Kitabu cha pili tulicho kiona kilikuwa kikubwa zaidi ya ile Bibilia.  Kilikuwa wazi na malaika alikuwa amekaa pale akiandika ndani yake.  Pamoja na Yesu , tulisogea karibu kuona nini mbacho malaika yule alikuwa.  Malaika alikuwa akiandika kila kitu kilicho kuwa kina tokea duniani.  Kila kitu kilicho tokea; pamoja na tarehe, saa, kila kitu kina andikwa pale.  Hili linafanyika ili neno la Mungu litimie pale linaposema na vitabu vikafunguliwa; kwamba watu juu ya nchi wakahukumiwa sawa na matendo yao yaliyo andikwa kwenye vitabu hivyo (Ufunuo 20:12).  Malaika alikuwa akiandika kila kitu ambacho watu walikuwa wakikifanya hapa duniani,kizuri au kibaya, vyote viliandikwa. 

Tuliendelea hadi kwenye kile kiitabu cha tatu.  Kilikuwa kibwa zaidi ya kile cha pili.Kitabu kilikuwa kimefungwa, lakini tulikisogelea.  Sisi sote 7, tulikichukua kile kitabu toka mahali pake, kutokana na amri ya Bwana, na tulikiweka juu ya nguzo. 
Nguzo zile nazile za miraba kule Mbinguni ni za ajabu sana!  Hazikufanywa kama kwa mawe duniani.  Nguzo zile za miraba zilikuwa kama za vito, zilikuwa zimefanywa kwa mawe ya dhamani. Baadhi zilikuwa zimefanywa kwa almasi, nyingine kwa emiradi, nyingine kwa dhahabu halisi na nyingine kwa mchanganyiko wa mawe ya aina tofauti. Niligundua kwa hakika kuwa Mungu ndiye mmiliki wa vitu vyote, kama ilivyo andikwa katika Hagai 2:8, "Dhahabu ni mali yangu, na fedha ni mali yangu." Nina elewa kuwa MunguI ni tajiri  sana na anamiliki utajiri wote duniani.  Nina elewa pia kuwa dunia na vyote viijazavyo ni mali ya Mungu wetu na anataka kuwapa wale wote wanao omba kwa imani
Bwana anasema, "Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa uridhi wako." (Zaburi 2:8)  Kitabu hiki ambacho tulikiweka kwenye zile nguzo, kilikuwa ni kikubwa sana kiasi kwamba kuweza kufungua ukurasa mmoja tulitembea hadi upande mwingine wa ukurasa.  Tulijaribu kusoma kile ambacho kilikuwa ndani ya kile kitabu, kama Bwana alivyo alivyo tuambia.  Mwanzoni ilikuwa ni vigumu kusoma kwa sababu ilikuwa imeandikwa kwa  njia ambayo hatuijui hivyo hatukuelwa. Ilikuwa ni tofauti na lugha yeyote ile ya duniani; kilikuwa ni kitu cha kimbinguni.  Lakini kwa msaada wa Roho Mtakatifu, tulipewa neeema ya kuelewa.Ni kama vile kitambaa kiliondolewa machoni mwetu na tuli weza kuyaelewa yale maaandaiko; vile vile kama lugha yetu. 
Tuliweza kuona kuwa majina yetu wote saba yalikuwa yame andikwa kwenye kile kitabu.Bwana alituambia kuwa kilikuwa ni kitabu cha uzima. (Ufunuo 3:5)  Tuligundua kuwa majina yaliyo kuwepo kwenye kile kitabu siyo yale tunayo tumia duniani; majina haya yalikuwa ni mapya, hivyo neno la Mungu l;iweze kutimia linaposema kuwa Atatupa majina mapya ambayo hakuna mtu yeyote anayelijua isipo kuw yule tuu anaye lipokea. (Ufunuo 2:17)
Kule mbinguni tuliweza kuyatamka majina yetu, lakini mara Bwana alipo tuleta duniani, majina yale yaliondolewa kwenye ufahamu wetu na rohoni mwetu.  Neno la Mungu ni la milele na litatimia. Rafiki zangu,Bibilia inasema, (Ufunuo 3:11) Usiruhusu mtu akaichukua taji yako, usiruhusu mtu yeyote akaondoa nafasi ambayo tayari Baba anayo tayari kwa ajili yako.  Mbinguni kuna vitu millioni nyingi sana ambavyo ni vya ajabu, hatuwezi kuvielezea kwa midomo yetu. Lakini nataka kukuambia kitu hiki, "Mungu anakusubiri!" Hatahivyo, ni kwa yule atakaye vumilia hadi mwisho ndiye atakaye okoka! (Mark 13:13)

--- (Ushuhuda wa pili, Ariel) ---
Wakati tulipo anza kwenda juu kwenye Ufalme wa mbinguni , tulifika eneo zuri lenye milango ya dhamani.Mbele ya Milango walikuwepo malaika waili.Walianza kuongea.Lakini maneno yao yakikuwa ni ya kimalaika na hatukuweza kujua kile walicho kuwa wakiongea.Lakinio Roho Mtakatifu alitupa ufahamu.Walikuwa wakitukaribisha.Bwana Yesu aliweka mkono wake kwenye milango na ikafunguka.Kama Yesu hakuwa pamoja nasi, tusingeweza kuingia Mbinguni.
Tulianza kufurahia kila kitu mbinguni.Tuliona mti mkubwa, Bibilia inaelezea mti huu kama  "Mti wa Uzima."  (Ufunuo 2:7)  Tulikwenda kwenye mto, na tuliona samaki wengi sana ndani.Kila kitu kilikuwa ni cha kushangaza kiasi kwamba mimi na rafiki zangu tuliingia ndani ya yale maji. Tulianza kuogelea chini ya yale maji.Tuliona samaki wakiogelea na kuigusa miili yetu.Hawakuwa wakituimbia kama ilivyo kawaida duniani; Uwepo wa Bwana ulituliza samaki.Samaki walituamini kwa sababu walijua kuwa tusinge waumiza. Nilikuwa nimebarikiwa sana na kushangazwa kiasi kwamba nilimshika mmoja wa wale samaki na kumtoa nje majini.Cha kushangaza ni kwamba yule samaki alikuwa mtulivu sana akiufurahia uwepo wa Bwana hata mikononi mwangu.Nili mrudisha samaki kwenye maji. 
Jesus on the white horseNiliweza kuona kwa mbali kwamba kulikuwa na farasi weupe Mbinguni,kama ilivyo andikwam katika neno la Mungu katika Ufunuo 19:11. "Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye mwaminifu na wa kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita."  Farasi wale ni wale amabo Bwana atawatumia atakapo kuja duniani kuwachukua watuwake, kanisa lake.Niliwaendea wale farasi na kuanza kuwagusa.Bwana alinifuata na aliniruhusu kumpanda mmoja wapo. 
Nilipo anza kumwendesha , nilisikia kitu ambacho sikuwahi kukisikia duniani.Nilianza kisikia amani, uhuru, upendo, utakatifu ambao mtu anaweza kuwa nao katika eno lile zuri.Nilianza kufurahia kila kitu ambacho macho yangu yalikiona.Nilitaka kufurahia kila kitu katika eneo lile zuri ambalo Bwana ameandaa kwa ajili yetu. 
The banquet tableTuliweza pia kuona meza ya sherehe ya harusi, kila kitu kilikuwa tayari kime andaliwa.Haina mwanzo wala mwisho.Tuliona viti vimeandaliwa kwa ajili yetu.Kulikwepo pia mataji ya uzima wa milele ambayo yalikuwa yapo tayari kwa ajili yetu.Tuliona vyakula vizuri vikiwa yatari kwa ajili ya wote watakao alikwa kwenye meza ya mwana kaondoo.
Malaika walikuwepo pale na vitambaa nyeupe kwa mavazi ambayo Bwana anatuandalia.  Nilishangaa sana nikiangalia vitu vyote hivi.Neno la Mungu linatuambia ni lazima tuupokee Ufalme wa Mungu kama watoto wadogo. (Mathayo 18:3)  Tulipo kuwa mbinguni tulikuwa kama watoto wadogo. Tulianza kufurahia kila kitu pale; maua, makazi... Bwana alituruhusu hata kuingia ndani ya yale makazi.

Baadaye Mungu alituchukua hadi kwenye eneo lenye watoto wengi.Bwana alikuwepo katikati yao na alianza kucheza nao.Alihakikisha kuwa anatumia muda wa kutosha na kila mmoja wao. na alifurahia kuwa pamoja nao.Tulimsogelea Bwana na kumuuliza, "Bwana je! hawa watoto ndio watakao kwenda kuzaliwa duniani?".  Bwana alijibu, "Hapana, hawa ni wale ambao mimba zao zilitolewa duniani".  Kwa kusikia vile,nilisiia kitu ndani yangu kilicho nifanya nitetemeke. 
Nilikumbuka kitu fulani ambacho nilikuwa nimekifanya huko nyuma,wakati ambapo sikumjua Bwana.  Kipindi kile nilikuwa na uhusiano na mwana mke na alipata mimba.  Alipo niambia kuwa kwamba alikuwa nja mzito, sikujua nini cha kufanya hivyo nilimwomba anipe muda ili nifanye maamuzi.Muda ulipita na nilipo kwenda kwake kumweleza maaamuzi yangu, ilikuwa tayari nimechelewa kwa sababu alikuwa tayari amechatoa ile mimba..  Hili liliweka doa kwenye maisha yangu. Hata baada ya kumpokea Yesu moyoni mwangu, utoaji mimba ule ulinifanya nisiweze kujisamehe.Lakini Mungu alifanya kitu siku ile, aliniruhusu kuingia eneo lile na aliniambia, "Ariel, unamwona yule msichana pale?Msichana yule ni mtoto wako."  Alipo niambia vile nilimwona msichana,nilisikia kidonda kilichokuwa ndani yangu kwa muda mrefu kikianza kupona.  Bwana aliniruhusu kutembea karibu yake na alinikaribia.Nilimchukua mikononi mwangu na niliyaona macho yake.Neno moja nilisikia toka kwenye kinywa chake,"Daddii".  Nilielewa na nilijisikia kuwa Mungu anayo rehema juu yangu na amenisamehe,lakini ilibidi nijifunze kujisamehe mwenyewe.
Rafiki yangu, yeyote anayesoma habari hii, nataka kukuambia jambo moja.Mungu amekwisha kukusamehe dhambi zako, sasa nilazima ujifunze kujisamehe wewe binafsi.  Ninampa Mungu shukrani kwa kuniruhusu kuushiriki ushuhuda huu na wewe.  Bwana Yesu nakupa wewe heshima na utukufuLord!  Ushuhuda huu ni wa Bwana,alituruhusu sisi kuupokea ufunuo huu. Nina tumaini kuwa kila mmoja wetu atakaye usoma atapokea baraka za ushuhuda huu na ataupeleka ili kuwabarikia na wengine wengi.
Mungu akubariki.
 

--- (Ushuhuda wa tatu) ---
(Ufunuo 21:4)
Naye atafuta kila chozi katika macho yao,wala mauti haita kuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
Wakati tulipo fika, malango haya makubwa yalitufungikia, na nilianza kuona bonde lilojaa maua.Maua yalikuwa ni mazuri na harufu yake ilikuwa ni ya kipekee.Tulianza kutembea na  kuzoelea uhuru kamili kuliko tulio wahi kuwa nao duniani.Tulisikia amani iliyo ujaza miyoyo yetu na tulipo yaangalia maua tuligundua kuwa yalikuwa ni ya kipekee; kila kiini cha ua kilikuwa tofauti,halisi na yenye rangi ya kipekee
Ndani ya moyo wangu, nilimwambia Bwana kuwa nilitaka kuwa na ua kama moja wapo ya haya.Bwana alitoa ishara ya kunikubalia, nilisogelea ua na kuanza kulivuta. Lakini hakuna kilicho tokea, sikuweza kuling,oa ua toka aridhini. Sikuweza hata kuvuta kiini cha ua hata majani yake toka kwenye ua.Baadaye Bwana alivunja ukimya na kusema, "Hapa kila kitu ni lazima kifanyike kwa upendo."  Aligusa ua na ua lilijiachilia lenyewe kwenye mikono ya Bwana . Baadaye alinipa lile ua.Tuliendelea kutembea na harufu ya maua bado ilikuwa pamoja nasi.
Tulifika eneo lenye milango mizuri sana inayo fuatana.Milango hii haikuja ya kawaida, ilikuwa ni kazi  ya usitadi mkubwa na kulikuwa na mawe ya dhamani yaliyo chimbiwa ndani yake. Milango ilifunguka na tuliingia ndani ya chumba kilicho kuwa na watu wengi.Kila mmoja alikuwa akikimbia hapa na pale akifanya maandalizi.Baadhi yao walibeba majohoro ya vitambaa vyeupe juu ya mabega yao mashine  zenye nyuzi za dhahabu, na bado wengine walikuwa wakibeba aina fulani ya sahani zenye kitu kama ngao ndani yake.Kila mmoja alikuwa akikimbia kwa jitihada
Tulimuuliza Bwana ni kwa nini kulikuwa na juhudi kubwa vile na haraka. Hivyo Bwana alimwamuru kijana mmoja kuja karibu.  Mtu huyu alikuwa na  johora la kitambaa  mabegani mwake. Alikuja na kumwangalia Bwana kwa heshima. Wakati Bwana alipo muuliza kwa nini alikuwa amebeba johora lile la kitambaa, alimwangalia Bwana na kusema, "Bwana unajua kitambaa hiki ni cha nini! Kitambaa kinatumika kutengezea mavazi ya walio kombolewa, avazi kwa ajili ya Bibi arusi mkuu." Katika kusikia hili, tulijisikia furaha kuu na amani.  Ufunuo 19:8 Inatuambia: "Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing,arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifuk."

Tulipo toka nje ya mahali pale , tulijisikia amani zaidi,kwa sababu lilikuwa ni jambo zuri kuona kuwa Bwana mwenyewe alikuwa akiandaa kitu kizuri kwa ajili yetu.  Analo eneo na muda kwa ajili yako kwa sababu wewe ni wa muhimu kwake. Tulipo toka nje ya mahali pale, macho yetu yalichuliwa  katika kila maelezo ya mbinguni. Ni kama kila kitu kilikuwa na uhai wake pekee yake, na kila kitu pale kilikuwa kina mpa Mungu utukufu.

Jesus with the ChildrenBaadaye tulikuja kwenye eneo lililokuwa na watoto milioni na milioni, wa kila umri. Walipo mwona Bwana, wote walitaka kumkumbatia, kusikia zaidi upendo wake, kwa sababu yeye ndiye upendo wao. Yesu aalikuwa ni upendo wa kila mtoto pale. Tulijisikia kama kulia tulipo ona jinsi Bwana alivyo mhudumia kila mmoja wa watoto wale, jinsi alivyo wa busu na kuishika mikono yao.  
 
 
Tuliona jinsi malaika walivyo kuja karibu na Bwana, wakimletea watoto, wakimletea watoto waliofunikwa na nguo maalumu.  Bwana aliwajali, aliwagusa,aliwapa busu juu ya upaji wa nyusso zao na baadaye malaika waliwarudisha.Tulimuuliza Bwana ni kwanini kulikuwa na watoto wengi vile pale, je watot hawa ndio watakao kwenda kutumwa duniani.Bwana alio nyesha kuguswa kwa muda, na alisema, "Hapana, watoto hawa hawatatumwa duniani! Hawa ni wale ambao  mimba zao zilitolewa duniani, ambao wazazi wao hawakupenda kuwa nao.Hawa ni watoto wangu na nina wapenda." Niliinamisha kichwa changu, hata sauti yangu ilitetemeka kuuliza swali kama lile.
Wakati ule ambao sikumjua Bwana , yeye ambaye ndiye maisha ya kweli,nilifanya makosa na kutenda dhambi kama wati wengine. Kati ya dhambi hizo ni ile ya kutoa mimba. Kuna wakati nilikuwepo mbele ya uso wa Bwana na nilimuuliza, "Bwana, je! mtoto yule aliye tolewa mimba yake zamani yupo hapa?".  Bwana alinijibu, "Ndio."  Nilianza kutembea upande mmoja wapo na nilimwona mtoto mzuri wa kiume.  Karibu ya miguu yake alisimama malaika. Malaika alikuwa akimtazama Bwana, na kijana yule alitugeuzia mgongo wake. 
Bwana aliniambia, "Angalia, yule ni mtoto wako."  Nilitaka kumwona hivyo nilimkiimbilia , lakini malaika alinisimamisha na mkono wake.Alini onyesha kuwa nilitakiwa kumsikiliza yule kijana kwanza. Nilianza kusikia kile yule mtoto alikuwa akisema .Alikuwa akiongea na kutazama upande ule wa watoto wengine. Alimuuliza malaika, "Je baba yangu na mama yangu watakuja mahali hapa mapema?"  Malaika, alini angalia, akamjibu, "Ndiyo,baba yako na mama yako karibu watauja sasa."
Sijui ni kwa nini nilipewa upendeleo wa kuyasikia maneno yale, lakini ndani ya moyo wangu nilijua kuwa maneno yale yalikuwa ni zawadi kubwa mabayo Bwana angeweza kunipa.  Mtoto huyu hakuwa akiongea kwa hasira, wala maumivu,labda kwa kujua kuwa hatukumruhusu azaliwe.Alikuwa akingojea tuu kwa upendo ambao Bwana alikuwa ameuweka moyoni mwake
Tuliendelea kutembea, lakini niliweka sura ya yule mtoto moyoni mwangu. Najua kuwa kila siku natakiwa kufanya jitihada kuhakikisha kuwa nitakuwa pamoja naye siku moja. Nina sababu moja nyingine ya kwenda pale, kwa sababu kuna mtu ananisubiri kwenye ufalme wa Mbinguni. Neno la Mungu lina tuambia katika Isaya 65:19, "Nami nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe  watu wangu; sauti ya kulia haitasikiwa ndani yake tena, wala sauti ya kuomboleza."
Tulikuja eneo lenye milima midogo, na Bwana Yesu alikuja huku akicheza. Mbele yake walikuwepo umati wa watu wakiwa wamevaa mavazi meupe na waliinyanyua mikono yao juu ikiwa na matawi mabichi ya mizeituni. Walipo yanyoosha yale matawi hewani, waliachilia mafuta.Mungu anakitu kikubwa alicho kiandaa kwa ajili yako! Sasa ni wakati wako wa kuandaa moyo wako kwa ajili yake.
Mungu akubariki.

--- (Ushuhuda wa nne) ---
Kwenye Ufalme wa mbinguni, tuliona vitu  vya ajabu kama ilivyo andikwa katika neno la Mungu, 1 Wakorintho 2:9, "Mambo ambayo jicho halikuyaona, wala sikio halikuyasikia, wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampenda."
Tulifika wasili kwenye ufalme wa mbinguni ilikuwa ni ya kuvutia na kustaajabisha kuona vitu vingi vile; vitu vingi sana na kuusikia utukufu wa Mungu. Ilikuwa ni ya kipekee sana;eneo lenye watoto wengi sana.Tuna weza kusema kuna watoto millioni nyingi eneo lile. 
Tuliwaona watoto wa umri tofauti tofauti, mbingu ilikuwa imegawanywa kwenye maeneo tofauti.Tuliona aina ya nyumba za kutunzia watoto wenye umri mdogo wa miaka kama 2-4 .Tuligundua kuwa watoto mbinguni huendelea kukua na pia kuna shule ambapo watoto hufundishwa neno la Mungu. Waalimu ni malaika na wanawafundisha watoto nyimbo za kuabudu na jinsi ya kumtukuza Bwana Yesu.
Wakati Bwana alipofika, tuliweza kuona furaha kuu ya mfalme wetu. Japo hatukuweza kuuona uso wake, tuliweza kuona tabasamu lake, lilijaza eneo lote lile . Alipo wasili, watoto wote walimkimbilia! Katikati ya watoto wote wale, tulimwona Maria, mama wa Bwana Yesu duniani. Ni mwanamke mwenye sura nzuri sana. Hatukumwona akiwa kwenye kiti cha enzi wala hakuna yeyote aliyekuwa akimwabudu. Alikuuwepo pale sawa kabisa na wanawake wengine walioko mbinguni,kama watu wengine duniani alitakiwa aweze kuupata wokovu wake. Alikuwa na vazi jeupe na mshipi wa dhahabu matitini mwake na nywele zake ndefu zilifika chini ya kifua .
Duniani, tumesikia watu wengi sana wakimwabudu Maria  kama mama wa Yesu , lakini nataka kukuambia kuwa neno la Mungu linasema, "Mimi ndimi njia na kweli na uzima ; mtu haji kwa baba, ila kwa njia ya mimi." (Yohana 14:6) Mlango pekee wa kuingia kwenye ufalme wa mbinguni ni Yesu wa Nazarethi.
Tuligundua pia kuwa hakuna jua wala mwezi. Neno la Mungu linasema katika Ufunuo 22:5 " Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwakuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele."
Tuliweza kuuona utukufu wa Mungu. Ni vigumu kuuelezea ubaya tulio uona kuzimu, lakini pia ni vigumu kuuelezea ukuu na uzuri wa vitu tulivyo viona na ukamilifu wa aliyevifanya. Tulipo kuwepo pale tulitaka kukimbia na kuona kila kitu.. Tuliweza kulala chini kwenyemajani, na tuliweza kuusikia utukufu wa Mungu. Mluzi mwororo; upepo mzuri ulio jali nyuso zetu, kilikuwa ni kitu cha kushangaza.
Katikati ya anga tuliweza kuona msalaba mkubwa wa dhahabu. Tunaamini kuwa hii haikuwa ni ishara ya sanamu bali ni ishara ina yo onyesha kuwa kwa kifo cha Yesu tuna mlango wa kuingilia kwenye Ufalme wa mbinguni.
Tuliendelea kutembea mbinguni.Lilikuwa ni jambo la kuvutia sana kutembea na Bwana Yesu Kristo . Pale tulijua kwa hakika  ni Mungu yupi tunaye mtumikia ...Yesu wa Nazarethi. Wengi wetu tuna waza kuwa kuna Mungu juu mbinguni anaye tusubiri tufanye dhambi ili aweze kutuadhibu na kutupeleka Kuzimu.Lakini hili si sawa.Tuliweza kuuona upande mwingine wa sura ya Yesu; Yesu  aliye rafii, Yesu anayelia unapolia .Yesu ni Mungu wa upendo mwenye huruma na rehema; Anatubeba mikononi mwake ili tuendelee kwenye njia ya Wokovu.
Bwana Yesu pia alituruhusu kukutana na Mtu aliye kwenye Bibilia . Tulikutana na Daudi, Mfalme Daudi aliye tajwa kwenye maandiko.. Ni mtu mzuri, mrefu na sura yake ina akisi  Utukufu wa Mungu . Muda wote tulipo kuwa kwenye Ufalme wa Mbinguni, kitu pekee ambacho mfalme Daudi alikuwa akikifanya ni kucheza, kucheza, kucheza na kumpa Mungu Utukugu wote na heshima.
Kwa wote wanao usoma ushuhuda huu, nataka kukuambia kuwa, kwenye neno la Mungu inasema kwenye Ufunuo 21:27  "Na ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo."  Na pia nataka kukuambia kuwa wenye nguvu ndio wanao uteka ufalme wa Mbinguni.
Mungu akubariki. 
 

--- (Ushuhuda wa tano) ---
(2 Wakorintho 5:10)
Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele za kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyo tenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.
New JerusalemKwenye Ufalme wa Mbinguni, tuliweza kuiona Yerusalemu Mpya ambayo Bibilia inatuelezea habari zake katika  Yohana 14:2, "Numbani kwa Baba yangu makao ni mengi;kama sivyo, ningaliwaambia;maana nakwenda kuwaandalia mahali."  Tuli weza kuuona mji na kuingia ndani yake, ni mji wa kweli na wa ajabu! Yesu alikwenda kutuandalia mji huu wa kuishi. 
Kwenye jiji lile, tuliweza kuona kuwa kila jumba lilikuwa na jina la mtu anaye limiliki mbele yake . Jiji hili bado halikaliwi na mtu yeyote, lakini lipo tayari kwa ajili yetu. Tuliruhusiwa kuingia ndani ya zile nyumba na kuona vitu vyote mle ndani. Lakini baada tuu ya kuondoka mle ndani tulisahaulishwa kila kitu tulicho kuwa tumekiona, kumbukumbu zote ziliondolewa. Hata hivyo tunaweza kukumbuka nguzo za nyumba zimepambwa na vito vya dhamani na zina aina tofauti ya mawe ya dhamani ndani yake.Pia kuna dhahabu halisi ndani yake.
Dhahabu ya Jiji lile ni kama vile Bibilia inavyo elezea; Ni angavu, na inayo ngaa sana. Dhahabu ya duniani haiwezi kulinganishwa na kwa uzuri na umbo la ile ya Mbinguni.
Baada ya hivi, tulichukuliwa hadi kwenye eneo lenye vyombo vingii sana. Ndani ya vile vyombo kulikuwepo na machozi kama vile barafu iliyo ganda. Haya ni machozi ambayo watu wa Mungu wameya mwaga wakiwa duniani mbele za Mung, siyo machozi ya malalamiko, bali machozi ya toba, machozi ya kiuungwana. Mungu huyahifadhi machozi haya kama kitu cha dhamani Mbinguni,kama vile ilivyo tajwa katika  Zaburi 56:8, "Umehesabu kutanga- tanga kwangu; Uyatie machozi yangu katika chupa yako;je hayamo katika kitabu chako? "

Tulifika eneo pia ambalo kuna malaika wengi sana. Japo mbinguni tuliweza kuona aina nyingi za malaika,, eneo hili lina aina maalumu tuu ya malaika.Tuliona kuwa Yesu, ana malaika maalum,u kwa kila mtu.Alituonyesha kuwa malaika wale wangekuwa na sisi kwa muda wote wa sisi kuwepo .Alitutambulisha kwa malaika aliye pewa kuwa nasisi. Tulikwenda kuwaangalia na kujua tabia zao , lakini Mungu alitunyima tusi waambie watu mambo haya. Tunasoma katika Zaburi 91:11, "Kwa kuwa atakuangizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote."

Tulikuja kwenye eneo lenye makabati mengi, ndani yake kulikuwa na maua ya aina tofauti. Baadhi ya maua yalichaua na, mazuri na yenye kung,aa . Lakini mengine yalikuwa yame inama na  yamesinyaa .Tulimuuliza Yesu ninini maana ya yale maua ? Alijibu "Ni kwa sababu maisha ya kila mmoja wenu ni kama  moja wapo ya maua haya." Alichukua moja wapo ya ua linalo ng,aa na kusema, "Ua hili lina onyesha aina ya uhusiano mlionao na mimi."  Aliliacha lile ua na kuchukua jingine lilo kuwa chini. Alisema, "Angalia, mtu huyu yupo chini kwa sababu anapitia majaribu au magumu.  Kuna kitu katika maisha kina cho ingilia mahusiano yetu na huyu mtu. Una fahamu kile ninacho fanya na maua haya yanapo kuwa chini ili kuya fanya kuchangamka na kuwa na afya tena?" Akachukua ua  mkononi mwake na alisema, "Nina dondosha chozi langu juu yake na nina liinua tena."  Tuliona ni kwa nguvu kiasi gani ua hili lilivyo weza kuwa na uhai tena na kuinuka na rangi zake zake kuanza kuonekana tena.
Baadaye alichukua moja wapo ya ua lililo sinyaa na alilitupa kwenye moto na kusema, "Angalia mtu huyu alinijua na ameniacha na kwenda mbali nami.Sasa amekufa bila ya kuwa na mimi na ametupwa motoni." (Yohana 15:5-6)

Tulipo ondoka pale, tuliona kasiri zuri kwa mbali. Hakuna hata mmoja aliye dhubutu kulisogelea kasiri lile, na tuna amini hivi ndiyo vile maandiko yanavyo sema  katika  Ufunuo 22:1, "Kisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kung,aa kama bilauri, ukitoka kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana  Kondoo."  Tuna amini kuwa kasiri lile lilikuwa karibu na uwepo na kiti cha enzi.

Wakati tuki yapitia yote hata kwenye Ufalme wa Mbinguni, tulikuwa na furahja kubwa sana miyoyoni mwetu, tulikuwa na amani ipitayo ufahamu wote. (Wafilipi 4:7) Tulielewa kama ilivyo andikwa katika 1 Petro 1:4, "tupate na uridhi usio haribika, usio na uchafu, usio nyauka, ulio tunzwa mbinguni kwa ajili yetu."

--- (Ushuhuda wa sita) ---
(Luka 22:30)
"mpate kula na kunywa mezani pangu katika Ufalme wangu; na kuketi katika vitivya enzi, huku mkiwa hukumu makabila 12 ya izraeli."
Kwenye eneo lile la ajabu, Mungu alituruhusu kuona eneo zuri na la ajabu sana  jumba la mapokezi ambalo hatuku wahi kufikiri kama lima weza kuwepo mahali popopte kwenye sayari yetu. Tuliona Kiti cha enzi kikubwa na tuliona viti viwili vya dhahabu  halisi na mawe ya dhamani ambayo hayapo popote dunaini. Mbele ya kiti kile kikubwa cha enzi kulikuwepo meza kubwa isiyo na mwisho, na juu yake kulikuwa na kitambaa cheupe. Kilikuwa ni cheupe sana kwamba hatukuweza kukilinganisha na kitu chochote duniani humu.Aina zote za vyakula vizuri na vya kipekee vilikuwepo mezani.Tuliona dhabibu kubwa kama usawa wa machungwa, ma Bwana Yesu alituruhusu kuonja baadhi yake. Bado tunaweza kukumbuka ladha yake, ni kitu cha kipekee sana! Kaka zangu na rafiki zangu huwezi kufikiria jinsi kila kitu kilivyo andaliwa tayari kwenye ufalme wa mbinguni na kile ambacho tayari Mungu amekwisha kuandalia.(1 Wakorintho 2:9)
Pia kwenye meza ile, Mungu alituruhusu kuuona ule Mkate, "Manna".Huu ulikuwa ni mkate wa Mungu ambao Bibilia inatuambia habari zake. Tuliruhusiwa kuufurahia ladha yake pamoja na mambo mengine mengi ya ajabu yasiyo patikana duniani.
Vitu hivi vinatusubiri kama uridhi wetu usio haribika Kwenye Ufalme wa Mbinguni.Tutafurahia  vitu vya kushangaza sana vya kipekee na vyakula vyenye ladha nzuri wakati tutakapo urithi Ufalme wa Mbinguni. Tulishangaa kuona kuwa viti vilikuwa vimeizunguka ile meza pande zote. Viti hivi vizuri vina majina kila kimoja. Tuliweza kusoma bila shida majina yetu katika viti vile, lakii majina yetu hayakuwa ni yale tunayo yatumia huku duniani. Yalikuwa ni majina mapya ambayo hakuna mtu yeyote anaye yajua ila sisi wenyewe.   ( Ufunuo 2:17)
Kile kilichoandikwa katika neno la Mungu kilitu shangaza, "Lakini msifurahi kwa vile pepo wanavyo watii, bali furahinikwa sababu majina yenu yameandikwa Mbinguni." (Luka 10:20)  Kulikuwa na viti vingi sana! Kuna nafasi kwa kila mmoja anayetaka kwenda kwenye ufalme wa Mbinguni.. kulikuwepo pia viti ambavyo viliondolewa kwenye meza.  Hii ina maana kuwa kuna wanaume na wanawake ambao walikuwa wamechoka kumtumikia Mungu, na majina yao yalifutwa kwenye Kitabu cha Uzima na walitengwa na Karamu ya Mwana Kondoo.

Mungu pia alituruhusu kuwaona watu walio kwenye Bibilia, watakatifu wa ajabu sana ambao tuna wasoma kwenye maandiko.Tulishangaa kumwona Ibrahimu. Ibrahimu alikuwa ni mzee sio kwa umbo lake wala kuonekana kwake. Alikuwa ni mzee kwa hekima aliyo kuwa nayo. Nywele za Ibrahimu zilikuwa nyeupe kabisa, lakini kila unywele ulikuwa ni kama kiooo au kama mng,ao wa almasi. Kilicho tushangaza zaidi ni kuona kuwa alikuwa kijana zaidi hata kuliko sisi.Mbinguni kila mmoja wetu atahuishwa upya na kuwa vijana. Tulishangazwa zaidi na maneno yake. Ibrahimu alituambia neno ambalo hatutakisahau.  Alitukaribisha kwenye Ufalme wa Mbinguni na alituambia kwamba ni muda mfupi ujao tutakuwa kwenye eneo lile, kwa sababu kuja kwake Bwana Yesu Kristo kuna karibia haraka sana.