Zaburi 150
Msifuni Bwana Kwa Ukuu Wake 
 1 Msifuni Bwana. 
Msifuni Mungu katika patakatifu pake, 
msifuni katika mbingu zake kuu. 
 2 Msifuni kwa matendo yake makuu, 
msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. 
 3 Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta, 
msifuni kwa kinubi na zeze, 
 4 msifuni kwa matari na kucheza, 
msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi, 
 5 msifuni kwa matoazi yaliayo, 
msifuni kwa matoazi yavumayo sana. 
 6 Kila chenye pumzi na kimsifu Bwana. 
Msifuni Bwana!