--- (Ushuhuda wa Kwanza 1) ---
Bibilia,neno la Mungu lipo wazi sana juu ya somo la Mbinguni
na Kuzimu. Kwenye eneo hili ambalo tumelisoma, Bwana anatuelezea juu ya
maeneo mawili: Mbinguni na Kuzimu, hukumu au wokovu. Hakuna eneo nje ya haya.
Hakuna Pagatori. Hakuna Limbo,eneo ambalo eti watu hufikia kwa muda halafu
baadaye waende Mbinguni; Bibilia ipo wazi sana juu ya hili.
(Aprili 11 1995)
Mungu alitupa ufunuo a mbao ungebadili maisha yetu yote. Ni
mara tuu tulikuwa tumeanza kufahamu juu ya Mungu na juu ya neno lake.Sisi ni
vijana saba ambao Munguametupa upendeleo na jukumu kubwa la kuushirikisha
ulimwengu ushuhuda huu.
Kila kitu kilianza majira kama ya saa nne asubuhi 4.00
Tulikuwa tunaomba na tulikuwa tuna jiandaa kwenda pikiniki baadaye siku ile
. Ghafla majira ya saa nne 4.00 asubuhi nguvu kuu ya mwanga mweupe
uliangaza kupitia dirisha mojawapo. Wakati mwanga ulipotokea, sisi sote kwa
haraka tulianza kuongea kwa lugha mpya na tulibatizwa na Roho Mtakatifu .
Kwenye muda ule, sisis sote tulishangazwa na kuogopeshwa na
kile tulicho kiona. Mwanga ule wa utukufu ulikuwa ukiimulika chumba chote.
Mwanha huu ulikuwa na nguvu kuliko mwanga wa jua. Katikakati ya ule mwanga,
tuliwaona malaika wengi wakiwa wamevaa mavazi meupe. Malaika hawa walikuwa
ni wazuri sana, warefu, na wenye mvuto wa sura.
Kari kati ya Malaika wale tuliona kitu cha kutushangaza --umbo
la mwanadamu. Umbo hili lilikuw ni la kiumbe maalumu sana, mtu aliye kuwa
amevaa nguo nyeupe sana Nywele zake ni kama nyuzi za dhahabu. Hatukuweza
kuuona uso wake kwa sababu ulikuwa unang,aa sana. Hata hivyo tuliweza kuuona
mshipi wa dhahabu ukiwa matiti mwake, na maandishi ya dhahabu yaliyosema: "Mfalme
wa wafalme na Bwana wa mabwana ." Alikuwa amevaa viatu vya
dhahabu halisi miguuni mwake, na uzuri wake haukuwa na mfano.Tulipo uona
uwepo wa mtu huyu wote kwa pamoja tulisujudu kwa kupiga magoti.
Baadaye tulianza kuisikia sauti yake.Ilikuwa ni ya kipekee na
ya ajabu sana;kila neno liliingia miyoyonimwetu kama vile upanga ukatao
kuwili; kama vile ilivyo andikwa katika neno la Mungu(Waebrania
4:12). Alizungumza nasi kwa wepes lakini kwa maneno yenye nguvu sana.
Tulisikia sauti yake ikisema nasi kuwa, "Watoto
wangu wadogo, msiogope, mimi ni Yesu wa Nazarethi, na nimewatembelea
kuwaonyesha mambo ya ajabu ili muweze kuyaonyesha na kuyaelezea kwenye, Miji,
Mataifa, majiji, makanisa na kila mahali. Pale nitakapo waambia mwende,
mtaenda, na pale nitakapo waambia msiende msiende."
Bibilia takatifu, neno la Mungu, linasema katika
Yoeli 2:28 "Hata itakuwa baaada ya hayo ya
kwamba nitamimina Roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu waume na
wake watatabiri ,wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono."
Huu ni wakati ambao Bwana anauandaa kwa kila mmoja.
Baadaye kitu kigeni kilitokea, mwamba ulitokea katikati ya
kile chumba, na Bwana ambaye tulikuwa pamoja naye, alitufanya kuingia ndani
ya ule mwamba.Mwamba ule ulikuwa na urefu wa karibu inchi saba hivi juu ya
sakafu, na shimo kubwa lilitokea pale sakafuni.Lilikuwa ni
kubwa,jeusi,mwanya au uwazi wa kutisha.Kwa haraka tuliweza kuwa juu ya ule
mwamba na kuzama chini kupitia ule uwazi sakafuni.Ilikuwa ni giza
nailituongoza hadi katikati ya dunia.
Wakati tulipo kuwa ndani ya giza lile baya, tuliogopa
sana!tulitishika sana kiasi kwamba tulimwambia Bwana, "Bwana hatutaki
kwenda eneo lile! Usitupeleke eneo lile Bwana! Tutoe mbali na eneo hili
Bwana!" Bwana alitujibu kwa sauti nzuri na ya huruma, "Uzoefu
huu ni wa muhimu sana ili muweze kuuona na kuwaelezea wengine."
Tulikuwa kwenye tanuru lenye sura kama ya pembe, na tulizubaa
kwa kuangalia vivuli, mapepo na maumbo yalikuwa yakihama toka eneo moja
kwenda jingine. Tuliendelea kwenda chini na chini zaidi.Ndani ya sekunde
chache tulikuwa tukijisikia watupu na uoga mwingi.
Baadaye tulifika kwenye baadhi ya mapango makubwa;kwenye
malango ya kutisha, kama vile njia panda. Hatukutaka kuingia mle
ndani.Tuligundua harufu ya kutisha na joto lilotutetemesha.Mara tulipoingia
tuliona vitu vya ajabu na maumbo ya kutisha. Eneo lote lilikuwa limezungukwa
na miali ya moto;na katikati ya ile mioto, kulikuwepo miili ya watu maelfu.
Walikuwa wakiteseka katika mateso makuu.Eneo lilikuwa ni la kuogopesha sana,
hatukutaka kuona kile tulichokuwa tunaonyeshwa.
Eneo hili lilikuwa limegawanyika katika maeneo tofauti ya
mateso na maumivu.Moja ya eneo la kwanza ambalo Bwana alituruhusu kuliona ni
"Bonde la sufuria la kupikia" kama tulivyoliita. Kulikuwa na
masufuria mamilioni.Masufuria haya yalikuwa yamelazwa usawa wa aridhi; kila
moja lilikuwa linatokota uji wa moto.Ndani ya kila moja ilikuwepo roho ya
mtu aliyekuwa amekufa na kwenda kuzimu.
Mara tuu zile roho zilipo mwona Bwana, zilianza kupiga kelele
na kulalamika, "Bwana, utuhurumie! Bwana nipe nafasi ya kutoka nje ya
eneo hili! Bwana, nitoe nje na nitauambia ulimwengu kwamba eneo hili ni la
kwecli!" Lakini Bwana hata hakuwatazama. Walikuwepo mamilioni ya
wanaume kwa wanawake na vujana eneo lile. Pia tuliwaona watu wandoa ya
jinsia moja na walevi kwenye mateso.Tuliwaona watu hawa wote wakipiga
makelele kwa maumivu.
Ilituogopesha kuona jinsi ambavyo miili yao ilikuwa
imeharibiwa. Minyoo ilikuwa inaingia na kutoka kupitia kwenye mafuvu ya
macho yao, ya midomo yao, na masikio; na ilikuwa ikijiingiza kwenye ngozi
kuingia miilini mwao. Hii inatimiza neno la Mungu lililo andikwa kwenye
kitabu cha
Isaya 66:24 "Nao watatoka nje na kuitizama
mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hawatakufa, wala moto wao
hautazimika; nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili."
Pia katika
Marko 9:44,"Ambamo humo funza wao hafi, wala
moto hauzimiki." Tulikuwa tumeogopeshwa na kile tulicho kuwa
tunakiona. Tuliona miali ya moto kama ya urefu wa inchi 9 mpaka 12 hivi.
Ndani ya kila mwali wa moto kulikuwepo na roho ya mtu aliye kufa na kwenda
kuzimu.
Bwana
alituruhusu kumwona mtu ambaye alikuwepo ndani ya mojawapo ya masufuria yale
ya moto. Alikuwa kichwa chini miguu juu na nyama za uso wake zilikuwa ziki
anguka chini kwa vipande. Alibaki akimwangalia Bwana kwa makini; na baadaye
alianza kupiga makelele na kuliitia jina la Yesu. Alisema, "Bwana
nihurumie! Bwana nipe nafasi! Bwana nitoe nje ya eneo hili!" Lakini
Bwana Yesu hakutaka kumwangalia.Yesu alimgeuzia mgongo wake. Wakati Yesu
alipo fanya hivyo, mtu yule alianza kulaani na kumtukana Bwana. Mtu huyu ni
John Lennon, mjumbe wa shetani wa kundi la mziki la "The Beatles." John
Lennon alikuwa ni mtu aliyefanya mizaha na kumtania Bwana wakati wa maisha
yake.Alisema kuwa Ukristo ungekwenda kutokomea na Yesu Kristo angesahaulika
na kila mmoja.Hata hivyo leo, mtu huyu yupo kuzimu na Yesu Kristo yuu hai!!
Ukristo pia hauja tokomea.
Tulipo anza kutembea kwenye ukingo wa eneo hili, roho
zilikuwa zikinyoosha mikono yao kwetu na kutaka rehema.Walimwomba Yesu
kuwaondoa ndani ya eneo lile, lakini Bwana hata hakuwaangalia.
Baadaye tulianza kwenda katika maeneo tofauti tofauti.
Tulifika katika eneo lenye kutisha zaidi kuzimu,mahali ambapo mateso makubwa
sana hufanyika; katikati ya kuzimu. Eneo lenye mchanganyiko mkubwa sana wa
mateso;mateso ambayo mwanadamu yeyote hawezi kamwe kuyaelezea. Watu pekee
hapa ni wale tuu ambao walimjua Yesu na neno la Mungu. Walikuwepo
wachungaji,wainjilisti,wamisionari na aina zote za watu ambao waliwahi
kumkubali Yesu na kuujua ukweli;lakini waliishi maisha ya pande mbili.
Walikuwepo pia wale waliorudi nyuma kiimanin; mateso yao
yalikuwa ni makubwa mara elfu zaidi ya wengine. Walikuwa wakipiga makelele
na kuomba rehema kwa Bwana, lakini neno la Bwana linassema katika kitabu chaWaebrania
10:26-27, "Maana kama tukifanya dhambi kusudi
baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya
dhambi; bali kuna kuitazamia hukumu kwenye kutisha, na ukali wa moto ulio
tayari kuwala wao wapingao."
Roho zile zilikuwepo pale kwa sababu zilihubiri,zilifunga ,
ziliimba,na kuinua mikono yao kanisani lakini mitaani na majumbani
walikuwwepo katika uasherati, uzinzi, uongo, unyanganyi. Hatuwezi
kumdanganya Mungu. Bibilia inasema kwake ambaye alipewa vingi, atadaiwa
vingi. (Luka
12:48)
Mungu baadaye alituruhusu kuwaona wanawake wawili ambao
walikuwa ni wakristo wakiwa duniani, lakini hawakuwahi kuishi maisha ya haki
mbele za Bwana Mmoja akamwambia mwenzake, "Wewe masikini mlaaniwa! ni
makosa yako kwamba nipo eneo hili! hukunihubiria Injili takatifu! na
kwasababu hukuniambia ukweli, nipo sasa hapa kuzimu!" Walisema maneno
haya katikati ya miali ya moto, na walichukiana kwasababu hakuna
upendo,rehema wala kusameheana kuzimu.
Kulikuwa na roho maelfu ya wale ambao waliwahi kulijua neno
la Mungu, lakini maisha yao hayakuwa safi mbele ya uwepo mtakatifu wa Bwana.
"Huwezi kucheza na Mungu wala na miali ya moto
wa kuzimu!" Bwana alisema. Pia alituambia, "Wana
wangu, mateso yote duniani kwa pamoja sii kitu,SII KITU, kulinganisha na
mateso yale mtu hupata katika eneo lile zuri la kuzimu."
Kama ni hatari kiasi hicho kwa yule anayeteseka kidogo kuzimu, ni mbaya
kiasi gani basi kwa yule aliyeko katikati ya kuzimu ? ambao waliwahi kulijua
neno la Bwana na kwenda mbali nalo. Baadaye Bwana alituambia kuwa wale wanao
weza kucheza na moto duniani sii hivyo kuzimu hawawezi kamwe.
Tuliendelea kutembea maeneo tofauti tofauti na Bwana
alituonyesha watu wa aina mbali mbali. Tuliweza kuona kuwa watu wote pale
walikuwa na aina kama sita za mateso. Kulikuwepo na roho zilizo teswa na
mapepo kwa aina zote za adhabu. Aina nyingine ni ufahamu wao uliosema, "Kumbuka
wakati walipo kuhubiria, kumbuka wakati ulipo sikia neno la Mungu, kumbuka
walipo kuambia habari za kuzimu na ulicheka juu ya hilo !" Ufahamu wao
wenyewe uliwatesa; kama vile minyoo ile iliyopita juu ya miili yao, kama
vile moto ule ulao ambao ni mkali mara elfu, elfu zaidi ya tunavyojua.Hii ni
zawadi ambayo shetani anayo kwa wote wanao mtafuta na kumfuata.
Neno la Bwana linasema katika
Ufunuo 21:8 "Bali waoga na wasioamini, na
wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na
waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakao moto na kiberiti.Hii
ndiyo mauti ya pili."
Baadaye Bwana alituonyesha mtu aliyeua watu sita. Watu wale
sita walikuwa wamemzunguka, na walikuwa wakimpigia kelele wakisema, "Ni
makosa yako kuwa tupo hapa wote, MAKOSA YAKO!" Muuaji alijitahidi
kufunika masikio yake kwasababu hakutaka kuwasikiliza, lakini hakuweza
kuepuka kusikia kwani kule kuzimu fahau zako zinakuwa hai zaidi.
Roho mahali pale zilikuwa zikiteseka kwa kiu ya maji isiyo
vumilika na kutoshelezwa kwa njia yeyote;Kama vile kwenye Bibilia habari za
Lazaro na yule tajiri. (Luka
16:19) Tajiri kule kuzimu alitaka tuu tone la maji, yangemtosha. Neno la
Bwana linasema katika
Isaya34:9, "Na vijito vyake vitageuzwa kuwa
lami, na mavumbi yake yatageuzwa kuwa kiberiti, na aridhi yake itakuwa lami
iwakayo."
Katika
eneo lile,kila roho ilikuwa katikati ya moto. Watu huona mfano wamaji ya mto
safi katikati ya moto na wanapo jaribu kuufikia, mito hiyo hugeuka kuwa
moto.Huona pia miti yenye matunda ambayo hutoa maji, lakini wanapo jaribu
kuchukua, huungua mikono yao na mapepo huwacheka.
Baadaye Mungu alituchukua baya zaidi ya maeneo mengine ambayo
tumewahi kuyaona. Tuliona ziwa la moto na kemikali. Upande mmoja wa lile
ziwa kulikuwepo na ziwa dogo zaidi. Ndani ya ziwa lile dogo, kulikuwepo
naroho, milioni, milioni, zikilia na kuomba kwa Bwana kuwa rehemu.
Walimwambia, "Bwana tafadhali! Tutoe nje ya eneo
hili hata kwa muda kidogo! Tafadhali nipe nafsi ya kwenda nje!!!"
Hatahivyo, Bwana hakuweza kufanya chochote kwa sababu hukumu yao tayri
ilisha pangwa.
Kati ya roho zile milioni na milioni, Bwana alituruhusu
kumwangalia mtu mmoja ambaye mwili wake nusu ulikuwa umezama katika ziwa la
moto.Bwana alituruhusu kuelewa na kuyafahamu mawazo yake.Jina la mtu huyu ni
Marko.Tulishangaa na yale mtu huyu aliyojisemea mwenyewe katika mawazo yake.
Tulijifunza somo ndani yetu tulipo yasikia mawazo yake yafuatayo, "Ningetoa
chochote kile kuwa katika nafasi yako sasa! Ningetoa kitu chochote ili
kwenda duniani kwa dakika moja tuu. Singejali kama ningekuwa na hali mbaya,
mgonjwa sana, ninayechukiwa sana, au mtu masikini kuliko wote duniani,
ningetoa chochote kuweza kwenda duniani! kwa dakika moja tuu duniani."
Bwana Yesu alikuwa ameushika mkono wangu. Yesu aliyajibu mawazo ya Mariko
kwa kusema, "Mariko, kwanini ungependa kurudi
duniani hata kwa dakika moja?" Kwa kulia na kwa sauti ya
mateso, alimwambia Yesu, "Bwana! nitatoa kitu chochote kuweza kurudi
duniani tuu kwa ajili ya kutubu na kuokoka."
Bwana aliposikia kile ambacho Mariko alisema, niliona
damuikitoka katika majeraha ya Yesu na machozi yaliyajaza macho yake na
alisema, "Mariko, umechelewa sana! Minyoo
imewekwa iwe kitanda chako na minyoo itakufunika." (Isaya
14:11) Wakati Bwana alipo mwambia hivyo, alizama kwenye ziwa lile
mojakwa moja. Ni kwa huzuni kuwa roho zile zote hazina tena tumaini. Ni sisi
tuu tuliopo duniani ambao tunayo nafasi ya kutubu leo na kwenda Mbinguni na
Bwana wetu Yesu Kristo.
Nina kuacha sasa na dada yangu kuendeleza ushuhuda huu,
asante.
--- (Ushuhuda wa pili 2, Lupe) ---
Mungu awbariki kaka zangu wapendwa.Tusome neno la Bwana
kutoka
Zaburi 18:9. "Aliziinamisha mbingu akashuka,
kukawa na giza kuu chini ya miguu yake" Wakati Bwana alipo
ifikia mikono yangu, niliishika mikono yake tulianza kushuka chini kupitia
tanuru lile.Tanuru lilikuwa linazidi kuwa giza na giza kiasi kuwa sikuweza
hata kuuona mkono wangu, ambao haukuwa umeushika mkono wa Bwana
Ghafla, tulikipita kitu fulani cheusi na chenye kutoa cheche;
kilikuwa kikitoa sauti.Giza lilikuwa kuu sana, mikono yako isdinge weza hata
kuguza kuta za lilr tanuru.. Tulishuka kwa kasi sana, kwamba nilisika kuwa
roho yangu ilikuwa ikitengwa na mwili wangu.
Mara nilihisi harufu mbaya ya kitu kilicho oza sana. Kama
harufu ya miili iliyo oza. Ilikuwa ikizidi kila mara. Baadaye nilisikia
sauti za mamilioni na mamilioni ya roho. Walikuwa bila kukoma wakipiga
makelele, wakilia, na kuhuzunika.Ilikuwa inaogopesha sana hivyo nilimgeukia
Bwana na kumuuliza, "Bwana , unatupeleka wapi? Bwana nirehemu!
Tafadhali nihurumie!" Bwana alisema tuu, "Ni
muhimu kwamba uone hili, ili uweze kumwaambia kila mmoja."
Tuliendelea
chini kupitia tanuru hili lenye sura ya pembe hata tulipo fika eneo ambalo
lilikuwa ni giza tupu. Kama vile kuondoa pazia zito machoni mwangu, baadaye
niliona miali ya moto milioni nba milioni.Kwa ubaya sana nilisikia sauti
zile maumivu lakini sikuweza kumwona yeyote. Niliogopa haswa. Nilimwambia
Bwana, "Oh tafadhali Bwana nirehemu!Ooh tafadhali Bwana unirehemu !
Usinipeleke eneo hili! Nisamehe!" Katika muda huu, sikujua tuu kuwa
mimi ni mtazamaji tuu wa kuzimu, nilifikiri ilikuwa ni siku ya mwisho.
Nikiwa nimesimama mbele ya Bwana Yesu, nilikuwa nikitetemeka kwa nguvu kwa
sababu nilifikiria kuwa ilikuwa ni mwisho wa maisha yangu.
Tulisogea karibu katika moto mkubwa mbele yetu; ulikuwa
mkubwa na uliwaka kwa ukali. Niliendelea kwenda chini taratibu, nikiona
miali ya moto mingi na kusikia sauti za mamilioni ya roho zilizo lia kwa
sauti kwa pamoja.
Baadaye
niliona meza ya mti ambayo haikufikiwa na moto.Kulikuwa na kitu kama chupa
za bia juu yake.Zilionekana kama ni za kuburudisha lakini zilijaa moto ndani
yake.Nilipo kuwa ninaangalia, mtu alitokea kw ghafla.Mwili wake ni kama
ulikuwa umekwisha na kile kilichokuwa kimebaki ni vazi lililo jaa tope na
moto. Alikuwa amepoteza macho yake, mdomo, na kila unywele kule motoni.
Aliweza kuniona bila hata macho yake.. Nina kuambaia huyu ni mtu anaye waza
, anayetafakari ,na kuona kwa kweli; sii kwa mwili wako wa asili.
Mtu huyu aliunyosha mkono wake kwa Bwana na kuanza kulia,
akisema,, "Bwana nirehemu! Bwana nirehemu! Nipo kwenye maumivu!
Ninaunguzwa! Tafadhali nirehemu na unitoe mahali hapa!" Bwana
alimwangalia kwa huruma,na nilianza kusikia kama joto kwenye mkonom
wangu.Niliangalia na kuona kuwa ni damu...damu ya Yesu! Damu ya Bwana
ilitoka mkononi mwake alipo kuwa akimwangalia mtu huyu akiteseka na
kuzungukwa na moto
Baadaye mtu huyu aligeuka na kuelekeza mawazo yake kwenye
meza na kutembea kuelekea zile chupa.Alichukua chupa na alipo kuwa karibu ya
kuinywa, moto na moshi ulitoka ndani ya ile chupa. Aligeuza kichwa chake
tena na ulia kwa jinsi ambavyo sijawahi tena kusikia..Alilia kwa maumivu
makuu sana na masononeko na alianza kunywa kile kilicho kuwepo ndani ya ile
chupa.Lakini chupa ile ilijaa asidi\ tindikali na koo lake liliaribiwa
karibu na kwisha. Ungeweza kuona tindikali ile ikipita mle tumboni na
kumuumiza.
Namba ile 666 ilikuwa imechimbiwa juu ya upaji wa uso wake.
Juu ya kifua chake kulikuwepo na sahani iliyo fanywa na malighafi isiyo
julikana mabyo hata ule moto wala minyoo isingeweza kuiangamiza. Ilikuwa na
maandishi juu yake lakini hatukuweza kuyaelewa Bwana kwa neeema yake kuu,
alitupa tafsiri ya kile kilicho kuwa kimeandikwa. "Nipo hapa kwa
sababu mimi ni mlevi." Alimwomba Bwana rehema,lakini neno la Mungu
lipo wazi sana linaposema katika
1 Wakotintho 6:10 "Wala wevi, wala watamanio,
wala walevi, wala watukanaji, wala wanyanganyi, hawatauridhi ufalme wa Mungu."
Mungu alinionyesha hali ya mtu huyu muda mfupi kabla hajafaa
duniani, kama vile sinema.Ilikuwa ni kama TV kubwa ikinionyesha sekunde
zake za mwisho kabla hajafa.Jina lake aliitwa Luis na alikuwepo baa akinywa
pombe. Niliona meza ileile na chupa ileile pale baa.Kuizunguka meza ile
walikuwepo marafiki zake. (Naweza kukuambia jambo hili sasa kuwa yupo
RAFIKI MMOJA TUU WA KWELI, na jina lake ni YESU KRISTO.Yeye ni rafiki
mwaminifu.) Luis alikuwa akinywa na marafiki zake walikuwa tayari
wamelewa. Rafiki yake mkubwa alichukua chupa na kuipasua na kuanza kumpiga
nayo Luis . Alipo onma Luis amelala chini alikimbia,na Luis alitokwa na damu
hadi kufa pale sakafuni. Jambo la huzuni sana ni kuwa alikufa bila Bwana
Yesu.
Katikati ya mambo haya yote, kwa jinsi roho zile zote zilivyo
kuwa zinalia, nilimuuliza Bwana, "Oh Bwana, tafadhali niambie je mtu huyu
alijua habari zako? Alifahamu habari za wokovu wako?" Bwana kwa huzuni
alijibu, "Ndiyo, Lupe, alijua habari zangu.
Alinipokea kama Bwana wake, lakini hakunitumikia." Baadaye
nilijisiki uwoga zaidi. Luis alilia kwa sauti na kupiga kelele"Bwana hii
inaumiza!inaumiza! tafadhali nirehemu!" Aliunyoosha mkono wake tena kwa
Bwana lakini Yesu aliuchukua mkono wangu na tulitembea kutoka eneo lile la
moto. Moto ulio muunguza Luis ulikuwa na ukali zaidi, na alilia kwa sauti
kuu zaidi, "Nirehemu! Nirehemu!!" Alitokomea baadaye kwenye ule
moto.
Tuliendelea kutembea, eneo hili lilikuwa kubwa na la
kuogopesha! Tuliufikia moto mwingine na nimwambia Bwana, "Bwana, hapana.!
Tafadhali sitaki kuona tena haya! nakuomba unisamehe!Tafadhali nisamehe!
sitaki kuona haya!" Hivyo niliyafunga macho yangu,lakini haikusaidia,
kufunga au kufungua bado niliona kila kitu.Moto huu ulianza kwenda chini
taratibu na baadaye nilimwona mwanamke.Alikuwa amefunikwa na tope, na tope
lilijaa minyoo mingi. Alikuwa bado na nywele chache zilizo baki na alikuwa
amezungukwa na minyoo pamoja na tope. Alikuwa analiwa na ile minyoo kila
eneo na alilia, "Bwana nirehemu! Bwana nirehemu na
unisamehe!niangalie.Hii inaumiza ! Nirehemu ! Niondolee hawa minyoo!Nitoe
ndani ya mateso haya kwa sababu yananiumiza sana!" Bwana alimwangalia
tuu kwa huzuni kuu . Tukiwa tumeshika mikono yake tuliweza kuhisi maumivu na
huzuni ndani ya moyo wa Yesu, kwa roho zote zinazo potea na kuchomwa milele
motoni kuzimu.
Mwanamke hakuwa na macho wala nyama midomoni, lakini aliweza
kuona na kuhisi ; maumivu yote yalikuwa ni makuu sana. Alikuwa na chupa
mkononi mwake, iliyo jaa tindikali, lakini aliamini kuwa ni manukato.
Niliweza kuona kuwa ni tindikali na kila mara alipo ipulizia mwilini mwake,
ilikuwa ikimuunguza. Hata hivyo aliendelea kuitumia ile tindikali tena na
tena.Aliendelea kusema kuwa ile ni manukato ya dhamani sana.Aliamini pia
kuwa alikuwa amevaa nguo isiyo na shingo, lakini kile nilicho kiona kiliwa
ni nyoka iliyo mzingira shingoni. Aliamini kuwa alikuwa amevaa ushanga wa
kupendeza sana, lakini niliona zilikuwa ni minyoo ya kweli kabisazenye urefu
wa kam futi moja wakiwa na hasira na kujichimbia ndani ya mifupa
yake.Alikuwa amevaa chapa ya chuma ambayo kila mmoja anayo kule kuzimu.
Iliandikwa, "Nipo hapa kwa ajili ya wizi."
Mwanamke huyu hajutii dhambi zake. Bwana alimuuliza, "Magdalena,
kwanini upo eneo hili,? Alijibu, "Haikunisumbua kuwaibia
wengine.Kile nilicho jali ni kupata vito vya dhamani na manukato za dhamani.
Sikujali ni nani niliye muibia, mradi tuu nipendeze."
Nili ushika mkono wa Kristo nilipo ona minyoo ikimwingia
mwilini mwake .Magdalena aligeuka akitafuta kitu fulani. Nilimuuliza Bwana
tena, "Bwana, je mtu huyu alikujua?" Na Bwana alijibu, "Ndiyo,
mtu huyu alinijua."
Magdalena alianza kuangalia pembeni, akisema, "Bwana, yupo
wapi mwanamke yule amliye ongea nami habari zako?Yupo wapi? Nimekuwepo hapa
kuzimu kwa miaka 15 sasa." Watu wote kuzimu wanaweza kukumbuka kila
kitu. Mgadalena aliendelea kusema, "Yupo wapi mwanamke huyu? Siwezi
kumwona!" Nilijua kuwa mwili wake usingeweza kugeuka kwasababu nyama za
ule mwili zingebaki mahali pamoja. Alijaribu kugeuka na kuangalia kwenye
mioto mingine, kumtafuta yule mwanamke aliye ongea naye juu ya Mungu. Bwana
alisema, "Hapana! hapana, Magdalena, hayupo
hapa. Yule mwanamke aliye kuambia habari zangu yupo kwenye Ufalme wa
Mbinguni pamoja nami."
Kwa kusikia hili, alijitupa wmenyewe chini ya ule moto ambao
ulimuunguza zaidi. Bango lake lilikuwa likimhukumu kuwa ni mwizi. Nataka
usome neno la Bwana katika
Isaya 3:24. "Hata itakuwa ya kuwa badala ya
manukato mazuri kutakuwa uvundo, na badala ya mishipi, kamba; na badala ya
nywele zilizo sukwa vizuri, upaa; badala ya kisibau mavazi ya gunia, na
kutiwa alama mwilini kwa moto badala ya uzuri."
Kwa jinsi tulivyo endelea kutembea na Bwana, niliona eneo la
miraba lililojaa minyoo.Kulizunguka kulikuwepo na chuma chenye moto
mwekundu.Kwenye eneo lile la miraba kulikuwepo na ubao ulio angaza kila
mahali . Ubao uliandikwa,"Karibuni waongo na wasengenyaji." Mwisho
wake kulikuwa na ziwa linalo tokota. Ilikuwa ni kama uji wa kikemikali unao
tokota. Baadaye niliwaona watu walio uchi kabisa wakija chini eneo lile.
Walipo kuwa wanateleza kuja ngozi zao zilikuwa zinabaki kwenye kile
chombo.Walipo angukia kwenye ziwa lile, ndimi zao zilitanuka hadi kupasuka
na minyoo ilitokea badala ya ndimi zile..Matezo yao yalianza. Neno la Mungu
linasema katika
Zaburi 73:18-19 "Hakika wewe huwaweka kwenye
utelezi, Huwaangusha mpaka palipo haribika. Namna gani ukiwa mara!
wametokomea na kutoweshwa kwa utisho."
Baada ya kuona hili, tulichukuliwa tena , nje ya kuzimu. Nina
taka kukuambia kuwa Mbingu na Kuzimu ni za kweli kuzidi hata ulimwengu wetu
huu tunao ujua. Ni hapa tuu unapo weza kuamua ni upande upi unao taka kwenda;
kuutumia umilele na Yesu au kuunguzwa kuzimu.Bwana aliendelea kutuambia,"Pasipo
utakatifu hakuna mtu atakaye niona mimi, pasipo utakatifu hakuna mtu atakaye
niona mimi." (Waebrania
12:14) Hii ndiyo sababu ninakuambia kitu kile kile sasa, "Pasipo
utakatifu hakuna mtu atakaye mwona Bwana."
--- (Ushuhuda wa tatu 3, Sandra) ---
Hebu twende pamoja kwenye neno la Bwana katika
Mathayo 10:28 " Msiwaogope wauao mwili,
wasiweze kuiua roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na
roho pia katika Jehanum."
Wakati roho inapo fika kuzimu, mtu huyo huchukua mwili wa
mauti.Bwana Yesu alinishika mkono wangu na tulianza kwenda chini kupitia
tanuru lenye giza kuu linaongoza kwenda katikati ya dunia. Tulifika eneo
lenye milango mingi; mmoja wao ulifunguka na tuliingia pamoja na Bwana.
Sikuweza kuuachia mkono wa Bwana maana nilijua kwa kufanya hivyo
ningelibakia mle kuzimu milele.
Baada
ya kuingia mlango ule, niliona ukuta mkubwa sana.Kulikuwa na watu kwa maelfu
waliokuwa wametundikwa vichwa vyao na komeo, na pingu zilizo wafunga mikono
yao ukutani. Tuliona pia maelfu ya watu wakiwa wamesimama katikati ya mioto
kila eneo.
Tulikwenda mbele ya ile mioto na mara ilianza kutulia
taratibu.Mara niliweza kumwona mtu mle ndani, na alipo ongea, niliweza kujua
kuwa alikuwa ni mtu.Mtu huyu alikuwa amevaa vazi la Kikuhani lililokuwa
limeharibiwa kabisa .Minyoo ilikuwa ikimwingia na kutoka.Alionekana mweuusi
kutokana na kuunguzwa na moto. Macho yalikuwa yamemtoka na nyama yake
ilikuwa imeyeyuka na kuanguka chini. Lakini baada ya nyama yote kuanguka
chini baadaye humrudia na tendo hili huanza tena.
Alipo mwona Yesu, alisema, "Bwana unirehemu,unirehemu! Tafadhali
nitoe hapa hata kwa kitambo kidogo tuu! kwa dakika tuu!" Kwenye kifua
chake lilikuwepo bango lilosomeka, "Nipo hapa kwa ajili ya wizi."
Wakati Yesu alipo kuja karibu, alimuuliza yule mtu,"Jina
lako ni nani?" Akajibu, "Andrea, jina langu ni Andrea,
Bwana." Bwana akamuuliza, "Ni kwa muda gani
umekuwepo hapa?" Andrea alijibu, "Nimekuwepo hapa kwa
muda mrefu sana." Mtu huyu alianza kuelezea habari za maisha yake.
Alisema, alikuwa na kazi ya kukusanya fungu la kumi na kupanga jinsi ya
kugawa fedha za kanisa lake la Katoliki kwa masikini.Hata hivyo,alikuwa
akiiba zile fedha. Kwa macho yaliyo jaa huruma, Bwana alimuuliza, "Andrea,
Uliwahi kuisikia injili ?" Andrea alijibu, "Ndio Bwana,
alikuwepo mwanamke mmoja wa kikristo aliye ingia kanisani na alihubiri
injili mara moja, lakini sikutaka kuipokea.Sikutaka kuiamini, lakini
naiamini sasa! Sasa naamini kuwa huu ni ukweli! tafadhali Bwana nitoe mahali
hapa,hata kwa kitambo tuu!"
Alipo kuwa akiongea, minyoo ilikuwa ikitambaa kwenye mafuvu
ya macho yake yakitokea masikioni, na kuingia tena kupitia mdomo wake.
Alijaribu kuwavuta nje kwa mikono yake lakini haikuwezekana. Alikuwa akipiga
makelele kwa na kumwomba Mungu amrehemu. Aliendelea kumwomba Yesu amtoe
mahali pale. Mbaya zaidi kulikuwepo na pepo linalo mtesa, muda wote
yakimchoma na mikuki yao.Pepo hili lilifanana na midoli ile tuliyo nayo hapa
duniani tunayo iita "Joridano". Niliiona midoli hiyo kuzimu, lakini
sasa haikuwa tena ni midoli;yalikuwa hai na ni mapepo. Yalikuwa ya urefu
karibu futi tatu na meno makli sana. Damu zinawatoka mdomoni na macho yao
yalikuwa ni mekundu kabisa.
Yalikuwa yakimsumbua Andrea kwa nguvu zao zote, pamoja na
wengine walio kuwepo eneo hili la kuzimu.. Nilipo ona hili, nilimuuliza
Bwana inawezekana je midoili ya duniani, kufanana kama yale mapepo.Bwana
aliniambia kuwa yale ni mapepo ya huzuni.
Tulipo endelea, tuliwaona maelfu ya watu kwenye mateso,Wakati
roho inapo mwona Bwana, zilijitahidi kumfikia kwa mikono isiyo na
ngozi.Nilimwona mwanamke aliye anza kupiga makelele alipo mwona Bwana Yesu.
Alilia, "Bwana tafadhali nirehemu! nitoe mahali hapa!" Alikuwa
akiteseka sana na aliunyoosha mkono wake kwa Bwana.Aliendelea kumwomba Bwana
amtoe eneo lile hata kwa sekundr moja. Alikuwa yuu uchi kabisa na
alifunikwa na tope. Nywele zake zilikuwa ni chafu na minyoo ilikuwa
ikijongea mwilini mwake .Alijaribu kuiondoakwa mikono yake lakini kila alipo
mwondoa mmoja mingine ilijizisha zaidi.Minyoo ilikuwa na urefu karibu inchi
6-8.Neno la Bwana linasema katika
Marko 9:44, "Ambamo humo funza wao hafi, wala
moto hauzimiki."
Ilikuwa ni ya kutisha sana kumwona mwanamke huyu na kusikia
kilio chake kwa jinsi minyoo ile kwa hasira ilivyo kuwa inaila nyama za mama
huyu. Kulikuwepo na bango la chuma lililo kifuani mwake ambalo lisingeweza
kuharibiwa na moto. Lilisomeka , "Nipo hapa kwa ajili ya Uzinzi."
Kwa jinsi ile ile ya dhambi yake, mwanamke huyu alilazimishwa kufanya uzinzi
kuzimu na nyoka wa kutisha mnene..Nyoka huyu alikuwa na miiba mikubwa
kuuzunguka mwili wake, ni kama ya uerfu wa inchi 6-8 hivi.Nyoka humwingia
mama hyu sehemu zake za siri na kusafiri hadi mwilini mwale hadi kwenye
koromeo lake. Nyoka alipo mwingilia hivi, alianza kulia kwa makelele .
Alimwomba Bwana kwa nguvu sana amtoe eneo lile, "Bwana,
nipo hapa kwa ajili ya uzinzi, nimekuwepo hapa kwa miaka 7, tangu UKIMWI
ulipo niua. Nilikuwa na wapenzi sita6, na nipo hapa kwa ajili ya uzinzi."
Kule kuzimu alitakiwa kuirudia dhambi yake tena na tena. Hakuna kupumzika
usiku na mchana, akiteseka kwa jinsi ile ile kila mara. Alijaribu kuunyoosha
mkono wake kwa Bwana, lakini Bwana alimwambi, "Blanca,
kwako tayari umechelewa. Minyoo itakuwa ni kitanda chako, na minyoo
itakufunika." (Isaya
14:11) Wakati Bwana alipo sema maneno hayo, blanketi la moto
lilimfunika, na siku mwona tena.
Tuliendelea
kutembea, tukiona maelfu na maelfu ya watu. Walikuwepo vijan, watu wazima na
wazee kabisa wakiteseka kuzimu. Tulifika eneo lililo onekana kama eneo la
bwawa la kuogelea la moto, likiwa na maelfu ya wanaume na wanawake ndani
yake. Kila mmoja wao alikuwa na bango la chuma kifuani mwake lililosomeka: "Nipo
hapa kwa kuto toa fungu la kumi na sadaka" Nilipo soma vile,nilimuuliza
Bwana, "Inawezekanaje hili kuwa hivi, kwamba mtu yupo hapa kwa sababu hii??"
Bwana alijibu,"Ndiyo, kwasababu watu hawa
walifikiri kuwa fungu la kumi na sadaka hazikuwa ni lazima, wakati neno
langu lina onyesha kuwa ni amri." Katika
Malaki 3:8-9 inasema "Je! mwanadamu atamwibia
Mungu? lakini ninyi mnaniibia mimi.Lakini ninyi mwasema .tumekuibia kwa
namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana
mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote."
Bwana aliniambia kuwa wakatim watu wake wanapo zuia fungu la
kumi, inazuia kazi ya Bwana, na injili haibiriwi. Watu wa eneo hili
wanateseka mara elfu zaidi ya wengine, kwa sababu, walilijua neno la Bwana
na hawakulitii.
Tuliendelea kutembea na Bwana alinionyesha mtu.Niliweza
kumwona kuanzia kiunoni hadi kichwani, na nilianza kuona maono ya jinsi
alivyo kufa. Jina lake ni Rogelio. Alikuwa ndani ya gari lake wakati mtu
alipo msogelea kumhubiria injili , na kumpa Bibilia . Lakini Rogelio
alikataa maonyo ya mtu yule na aliendelea kwenye njia yake, bila ya kujua
kuwa dakika chache baadaye gari lake linge pata ajali. Liliangukia kwenye
korongo, na mara alikufa.
Mara tuu baada ya ajali, Bibilia ilifunguliwa katika
Ufunuo 21:8, "Bali waoga, na wasioamini,na
wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na wahao waabuo sanamu, na
waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii
ndiyo mauti ya pili." Wakati Rogelio aliposoma msitari huu,
alikufa na alifika kuzimu.
Alikuwepo pale mwezi mmoja tuu na bado alikuwa na ngozi usoni
mwake. Hata hivyo alikuwa akiteseka kama wengine. Mwanzo hakujua ni kwanini
alikuwepo kuzimu. Nafikiri yule mkristo alipo mfikia pale kwenye gari yakr,
ilikuwa ndiyo nafasi yake ya kipekee na ya mwisho ya kumkubali Bwana Yesu.
Kwa jinsi ile ile ambayo wengi wamepata nafasi ya kumkubali Yesu.Leo nina
kualika ufungue moyo wako kwa Yesu; Yeye tuu ndiye njia,kweli, na uzima. (Yohana
14:6) Ni kwa yeye tuu tunaweza kuokolewa kuingia ufalme wa Mbinguni (Matendo
4:12) Bwana alituambia pia kuwa tuzifuate njia zake katika utakatifu na
heshima. Mungu akubarik
--- (Ushuhuda wa 4) ---
Mungu awabariki kaka zangu. Wakati Bwana alipo uchukua mkono
wangu, niliweza kuona kuwa nilikuwa nimesimama kwenye mwamba, na nyuma yetu
nilimwona malaika. Tulianza kwenda chini kupitia tanuru lile kwa mwendo wa
kasi wa kutisha.Kwa haraka, niligeuka na kuona kuwa malaika alikuwa
ameondoka, na nilijisikia hofu.Nilimuuliza Bwana, "Bwana, yupo wapi yule
malaika? kwanini hayupo hapa tena?" Bwana alisema, "Hawezi
kwenda pale sisi tunapo kwenda."
Tuliendelea kwenda chini naghafla tulisimama, kama kwenye
lifti. Niliona matanuru kadhaa; na tuliingia mojawapo ambalo dada yangu
Sandra ameshalizungumzia tayari. Pango ambalo watu walikuwa wametundikwa
wakining`inia na pingu mikononi mwao. Ukuta ambao ulikuwa na watu juu yake
ulikuwa ni mrefu usio na mwisho. Mamilioni ya watu walikuwa pale
wakining`inia . Walikuwa na minyoo mwili mzima. Niliangalia mbele na liona
kuwa kulikuwa na ukuta mwingine, kama ule mwingine. Nilimwambia Bwana, "Bwana!
Kuna watu wengi sana eneo hili!" Mara, andiko liliingia akilini
mwangu;ambalo silikumbuki. Bwana aliniambia, "Kuzimu
na uharibifu havishibi." (Mithali
27:20)
Tulitoka
pale na mara tulifika eneo linaloitwa, "Bonde la Masufuria ya
moto(cauldrons)". Masufuria haya yalijaa matope yanayo tokota, na
tulilisogelea moja wapo. Mtu wa kwanza ambaye nilimwona alikuwa ni mwanamke.
Mwili wake ulikuwa ukipanda juu na kushuka chini katika tope lile linalo
tokota la moto, lakini Bwana alipo mwangalia aliacha kwenda na alibaki
akielea kuanzia kiunoni kwenda juu. Bwana alimuuliza, "Mwanamke,
jina lako ni nani?" Alijibu, "Jina langu ni Rubiella."
Nywele zake zilijaa matope yanayo tokota na nyama za mwili
wake zilikuwa zina ning`inia toka mifupa yake, ambayo ilikuwa mweusi kwa
kuunguzwa. Minyoo ilimwingia kupitia mashimo ya macho yake, ikitoka kupitia
midomo yake, ikiingia tena kupitia pua zake na kutokea masikioni. Wakati
minyoo ilipo shindwa kuingia, ilifanya shimo yenyewe kupitia eneo jingine la
mwili, ambayo ilisababisha maumivu yasiyo elezeka.
Alipiga makelel, "Bwana, tafadhali! Nitoe mahali hapa.
Nirehemuu! siwezi kuendelea jinsi hii tena! isimamishe Bwana! siwezi
kuendelea tena!tafadhali nirehemu!." Bwana alimuuliza ni kwa nini
alikuwepo pale.Alisema kuwa alikuwepo pale kwa sababu ya maringo, kitu
ambacho ni saw na jinsi ilivyo kuwa imeandikwa juu ya bango lake lililo
kifuani mwake.Mkonoi mwake ni chupa ya kawaida, lakini kwake aliiona kama ni
manukato ya dhamani kubwa. Rubiella angechukua chupa ile iliyojaa tindikali
, na angejipulizia mwili wake wote. Hii ilimsababishia nyama yote iliyo
puliziwa kuyeyuka kumsababishia maumivu makubwa sana.
Alipiga kelele kwa Bwana, "Bwana tafadhali, nirehemu!
siwezi kuwepo tena hapa ! kwa sekunde moja tuu Bwana." Sisemi kuwa ni
dhambi kutumia manukato, lakini Bwana alituambia kuwa mwanamke yule
alikuwepo pale kwa ajili ya maukato yake, kama vile neno la Mungu linavyo
tuambia katikaI am not saying that it is a sin to use a perfume, but the
Lord told us that the woman was there because of her perfume, as the Word of
the Lord tells us in
Kumbukumbu la Torati 5:7 " Usiwe na miungu
mingine ila mimi." Alikuwepo pale kwasababu ya uzuri wake,
manukato, na maringo yalikuwa ndicho kitu cha kwanza katika maisha yake.
Hata hivyo, Bwana Yesu ni mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana! Anatakiwa
kuwa wa kwanza katika maisha yako; hii ndiyo maana alikuwepo pale. Kwa
huzuni, Bwana alimwangalia na kusema , "Rubiella,
unechelewa, minyoo itakuwa kitanda chako, na minyoo itakufunika."
Wakati Bwana aliposema hivyo, blanketi la moto lilimfunika kabisa. Wakati
wmili wake ukiwa umefunikwa kabisa ndani ya sufuria lile la moto, alikuwa
akitesema sana.
Tulitoka pale na kwenda mbali zaidi eneo lenye milango
imkubwa .Tulipokuwa tumeifikia, ilitufungukia yenyewe. Upande mwingine
tuliona pango kubwa. Nilipo angalia juu niliona rangi tofauti za mwanga
zikitembea kama mawingu ya moshi.Ghafla tulisikia mziki wac; salsa,
ballenato, rocki, na aina tofauti ya miziki mashuhuri ambayo watu
huisikiliza kwenye redio. Bwana aliuelekeza mkono wake na tuliona, mamilioni
na mamilioni ya watu wakiwa wametundikwa na minyororo mikononi mwao.
Walikuwa wakiruka ruka kama wanyama ndani ya moto.
Bwana alituangalia na alisema: "Angalia
huu ni mshahara wa wacheza mziki." Watakuwa wakiruka kama
wanyama juu na chini sawa na mapigo ya miziki. Kama ni salsa inapigwa,
walitakiwa kuruka kwa mapigo yale, kama aina nyingine ya mziki ikipigwa,
walitakiwa kuruka sawa na mapigo yake.Hawawezi kamwe kuacha kuruka.Lakini
mbaya zaidi, viatu vyao vina misumazi ya inchi6 chini yake. Wakati
wanaporuka inawangia miguuni mwao na hawatakuwa na nafasi ya
kupumzika.Wakati mtu anapotaka kuacha, pepo lingekuja maramoja na kumchoma
na mkuki, likiwalaani na kusema, "Msifuni yeye sasa!
Huu ndio ufalme wenu sasa, msifuni Shetani! msifuni! huwezi kuacha,
msifuni!ni lazima umsifu !lazima uruke! lazima ucheze!Uwezi kuacha hata kwa
sekunde moja."
Ilikuwa hatari kuwa wengi wa watu wale walikuwa ni wakristo
waliomjua Bwana,lakini walikuwa kwenye madisko ya usiku walipo kufa. Labda
unauliza, "Wapi Bibilia inasema kwamba ni vibaya kucheza?" Katika
Yakobo 4:4, Neno la Bwana linasema:: " Enyi wazinzi,
hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui na Mungu? basi kila
atakaye kuwa rafiki wa dunia kuwa adui wa Mungu." Pia katika
1 Yohana 2:15-17, "Msiipende dunia, wala mambo
yaliyopo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake,
maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na
kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.Na dunia
ianpita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu
hata milele." Kumbuka dunia itapita, vitu vyote hivi
vitaharibika, lakini yule atendaye mapenzi ya Mungu atadumu milele.
Rafiki zangu na kaka zangu, tulipo acha eneo hili, tuliona
kitu kama daraja lililo igawanya kuzimu katika maeneo tofauti ya
mateso.Tuliiona roho ikipita kwa miguu juu ya daraja. Ilionekana sawa na
mdoli tuliyo iona duniani; tunaiita mikokoteni ya dhamani. Ina nywele za
rangi za aina mbali mbali, zina nyuso za mzee lakini mwili wa mtoto, bila
maeneo ya siri. Macho yaliyo jaa uovu. Bwana alituelezea kuwa hizi ni roho
za upotovu. Roho hii ilikuwa na mkuki mikononi na ilikuwa ikitembea kwa
maringo katika daraja lile kama vile ni mwana wa mfalme.
Alipo kuwa anatembea, aliwachoma watu chini kwa ule mkuki
wake. Alikuwa akiwalaani akisema,"Mnakumbuka siku
zile mlipo kuwa nje ya makanisa ya kikristo na mlikataa kuingia ndani?
Mnakumbuka siku zile walipo wahubiria na hamkutaka kusikiliza? Mnakumbuka
wakati walipo wagawia vipeperushi vya injili na mkavitupa mbali?"
Roho hizi zilizo potea hujitahidi kufunika maeneo yakle ambayo masikio hukaa.
Huwajibu mapepo yale, "Nyamaza! Nyamaza! usiniambie tena! sitaki kujua
zaidi, nyamaza!" Hata hivyo, mapepo yale hupenda kufanya vile kwakuwa
huwaingizia maumivu watu wale kwenye nafsi zao.
Tuliendelea
kutembea na Bwana. Kwa kule kuangalia umati wa watu, tuligundua kuwa mtu
mmoja alikuwa akipiga makelele zaidi ya wengine waliokuwa wakiungua
pale.Alikuwa akisema, "Baba, Baba, nirehemu!" Bwana alikuwa
asisimane lakini aliposikia neno "Baba" Alisisimka na kugeuka. Yesu
alimwangalia na kumuuliza,"Baba? Unaniita Baba?
Hapana, mimi siyo Baba yako na wewe kamwe sio mtoto wangu. Kama ungekuwa
mtoto wangu, ungekuwa sasa na mimi katika Ufalme wa Mbinguni.Ninyi ni wana
wa Shetani baba yenu." Ghafla blanketi la moto lilikuja na
kabisa lilimfunika mwili wake.
Bwana alituelezea habari ya maisha ya mtu yule. Mtu yule
alimwita Baba kwa sababu aliwahi kumjua . Alikuwa akienda kanisani na
alikuwa akilisikiliza neno la Mungu, na alikuwa amepokea ahadi nyingi za
Mungu. Hivyo tuliuliza, "Nini basi kilitokea Bwana? Kwanini basi yupo
hapa leo?" Bwana alitujibu, "Alikuwa
akiishi maisha ya aina mbili; moja nyumbani moja kanisani. Alifikiria moyoni
mwake, 'Hapana mtu anaye ishi karibu yangu, sii mchungaji, wala ndugu yeyote,
hivyo naweza kufanya chochote ninacho taka. Lakini alisahau kuwa jicho la
Bwana lipo juu ya njia zetu zote kwamba hakuna mtu anaye weza kumdanganya au
kujificha mbele za Bwana."
Neno la Bwana linatuambia kuwa, "Msidanganyike,
Mungu hadhihakiwi; Kwakuwa chochcote apandacho mtu, ndicho atakacho vuna."
(Wagalatia
6:7) Mtu huyu alikuwa akiteseka mara alfu zaidi ya wengine. Alikuwa
akilipwa hukumu mara mbili: moja kwa ajili ya dhambi zake na nyingine ni
kule kufikiri kuwa anaweza kumdanganmya Bwana.
Leo, watu wana jaribu kupima ukubwa wa dhambi; wanafikiri
kuwa kulawitiana, kuua ni dhambi kubwa zaidi ya kusema uongo au kusengenya.
Lakini mbele ya macho ya Bwana, dhambi zote hizi zina uzito mmoja na malipo
sawa. Bibilia inatuiambia kuwa, "Mshahara wa dhambi
ni mauti" "na roho itendayo dhambi ndiyo itakayo kufa." (Warumi
6:23) (Ezekieli
18:20) Rafiki zangu na kaka zangu, nina waalika sasa kuukubali mwaliko
wa Yesu. Yesu ameunyoosha mkono wake wa rehema kwako kama ukitubu.Neno la
Bwana linatuambia kwamba yule atakaye geuza njia zake na kutubu atapokea
rehema.Ni vizuri zaidi ukaamini sasa, kuliko kusubiri na kukuta njia ngumu
mbeleni. Mungu akubariki.
--- (Ushuhuda wa 5) ---
Neno la Mungu linasema katika
Warumi 6:23 " Kwa maaana mshahara wa dhambi ni
mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu."
Tulipo kwenda chini mahali pale, nilisikia maumivu na uzoefu
wa kifo. Nilikuwa nimeogopeshwa sana na kile nilicho kiona.Niligundua kuwa
kuliwa na watu wengi, wengi sana ; wote walikuwa wakilia na kupiga
makelele.Lilikuwa ni giza tupu, , lakini katika uwepo wa Bwana,giza
lilitoweka.Tuliona maelfu na maelfu ya roho zote zikilia kuomba msaada na
rehema.Walikuwa wakilia kwa Bwana kuwaondoa eneo lile. Tulijisikia pia
maumivu kwa sababu tulijua Bwana alikuwa akiteseka sana kila alipo waona.
Wengi walilia kwa Bwana kuwaondoa mahali pale angalau kwa
sekunde moja tuu. Bwana angewauliza, "Kwa nini
unataka kutoka nje ya hapa?", na wangelijibu, "Kwa sababu
ninataka kuokoka! Nataka kutubu na kuokoka!" Hata hivyo ilikuwa kwao
tayari wamechelewa.
Wapendwa watu mnaonisikiliza sasa, sasa ndio nafasi pekee ya
sisi kuchagua eneo letu la umilele. Unaweza tuu kuchagua umilele wa wokovu
au wa hukumu.
Tulikwenda chini kwa zaidi. Niliona kuwa sakafu tuliyokuwa
tunatembea juu yake, ilikuwa imeharibiwa na moto; na tope na moto lilikuwa
linatoka ndani yake. Kulikuwepo pia na harufu ya kutisha kila mahali.
Tulijisikia vibaya sana na mahangaiko kutokana na harufu na makelele ya watu
wote.
Tulimwona
mtu, kwa mbali ambaye alikuwa amezama chini kwenye tope la moto.Alipo toa
mkono wake. nyama toka toka mifupa yake zilidondoka chini kwenye
tope.Tuliweza kuona mvuke wa kikahawia ndani ya mifupa yake, hivyo
tulimuuliza Bwana ninini kile. Aina hii ya mvule upo ndani ya kila mtu
kuzimu.Bwana alituambia ni nafsi zao zilizokamatwa ndani ya miili yenye
dhambi; Kama ilivyo andikwa katika
Ufunuo 14:11 "Na moshi wa maumivu yao hupanda
juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, nao
wamsujudia huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake."
Tulianza kuelewa vitu vingi ambavyo tulividharau
duniani;Jambo la muhimu, ujumbe wa karibu zaidi ni kuwa, maisha yetu duniani
yana amua ni wapi tutakapo tumikia umilele wetu baada ya kufa.
Tulipo kuwa tunatembea tukiwa tumeshikana mkono na Bwana,
tuligundua kuwa kuzimu ina sehemu nyingi sana yenye mateso mbalimbali.
Tulifika eneo lenye vyumba vingi na roho nyingi zinateseka huko. Roho hizi
zilikuwa zinateswa na mapepo mengi ya aina nyingi. Mapepo yangeweza
kuzilaani zile roho, kwa kusema, "Ninyi masikini
mlio laaniwa, msifuni Shetani! Mtumikieni kama vile mlivyo fanya mlipo kuwa
duniani.!" Roho zile ziliteseka sana kutokana na minyoo ile; na
moto ulikuwa ni kama tindikali juu ya mwili wote.
Tuliwaona watu wawili ndani ya chumba kile cha jela, kila
mmoja alikuwa ameshika kisu na anamsumbua mwenzake. Wangelisema, "Wewe
masikini mlaaniwa! ni kwasababu yako ndiyo maana nipo hapa! Ulinifanya nije
hapa kwasababu ulinipofusha nisujue ukweli na hukuniruhusu kumjua Bwana!
Hukuniruhusu kumpokea! Mara nyingi nilipata nafasi lakini hukuniruhusu
kumkubali! Ndiyo sababu nipo hapa leo, nateswa usiki na mchana!"
Kupitia maono, Bwana alituonyesha maisha yao duniani,
Tuliwaona wakiwa baa ya pombe pamoja. Mazungumzo yalianza yaliyo pelekea
kupigana. Walikuwa tayari walevi. Mmoja alichukua chupa iliyo vunjika na
mwingine alitoa kisu. Walipigana mpaka wote wakawa wamejeruhiwa sana na
wakafa.Watu hawa wawili waliwekewa kulirudia tukio hili milele.Waliteseka
pia na kumbu kumbu zao kuwa walikuwa ni marafiki sana duniani, kama mtu na
nduguye wakipendana.
Nataka kukuambia leo kuwa, kuna rafiki mmoja tuu wa kweli,
na jiana lake ni Yesu wa Nazarethi . Yeye ni rafiki wa kweli. Ni rafiki
mwaminifu, aliye pamoja nawewe katika muda wote.
Tulipo endelea kutembea tulimwona mwanamke ndani ya chumba
kingine, alikuwa akinivingirisha kwenye lile tope. Nywele zake zilikuwa
chafu na zenye tope. Ndani ya chumba kile alikuwepo nyoka mnene
mkubwa.Alikuwa anamsogelea na kumzunguka mwili wake, na alianza kumwingilia
mwilini mwake akianzia sehemu zake za siri. Alilazimishwa kufanya uzinzi na
yule nyoka. Kwenye eneo hili, wanaume na wanawake waliokuwa wazinzi
walilazimishwa kufanya uzinzi . Hata hivyo walilazimika kufanya hivyo na
majoka yale yaliyofunikwa na vitu vikali mwili mzima kama chuma kikali cha
inchi 6. Nyoka aliuharibu kabisa mwili wa mwanamke yule kila mara alipo
mwingilia. Alilia sana kwa Bwana na kumwomba kusimamisha hali ile.Hakutaka
kuteseka tena. "Simamisha! Sitaki kufanya tena!tafadhali simamisha hii
hal!" Alimwomba Bwana amhurumie kila wakati nyoka alipo mwingilia na
muuharibu mwili wake tena na tena.
Tulijitahidi kuyafunga masikio yetu tusisikie kilio chake,
lakini bado tulimsikia.Tulijaribu kwa nguvu zaidi kufunga masikio yetu ,
lakini haikusaidia. Tulisema Bwana, "Tafadhali Bwana, hatutaki kuona na
kusikia hivi tena! tafadhali!" Bwana alitujibu, "Ni
muhimu muone haya, ili muwaeleze wengine. kwa sababu watu wangu
wanaangamizwa, watu wangu wanaukataa wokovu halisi, njia ya kweli ya wokovu."
Tuliendelea kutembea na tuliona ziwa kubwa lenye watu maelfu
na maelfu ndani yake katikati ya mioto.Walitupungia wakiomba msaada, lakini
kulikuwa na mapepo mengi yakiruka juu ya eneo lile.Mapepo haya yalikuwa
yanatumia mikuki yenye vichwa kama S- kuwaumiza watu wale waliokuwa
wakiunguzwa katika lile ziwa. Mapepo yaliwatania na kuwalaani yakisema, "Ninyi
masikini mlio laaniwa! Sasa ni lazima kumwabudu Shetani! Msifuni, msifuni
kama mlivyo fanya wakati mlipo kuwa duniani!" Kulikuwepo watu
maelfu kwa maelfu. Tuliogopa sana,tulihisi kama tusingeushika mkono wa Bwana
tungebaki katika eneo lile la kutisha. Tuliogopeshwa na vitu tulivyo kuwa
tunavihisi.
Kwa mbali tulimwona mtu aliyesimama, akiwa kwenye maumivu
makubwa na huzuni. Alikuwa na mapepo mawili yakiruka juu yake yakimtesa.
Yangeweza kuchimbia mikuki yao mwilini mwake na kutoa mbavu zake. Yalikuwa
pia yakimtania kila mara. Zaidi ya yote Bwana alinionyesha kuwa alikuwa
akiteseka kwa hofu ya kila siku juu ya familia yake aliyo iacha duniani. Mtu
huyu hakutaka familia yake ije mahali pale pa mateso. Aliogopa kwa sababu
hakuwahi kuwapa ujumbe wa wokovu. Aliteseka zaidi kwa kukumbuka kuwa wakati
fulani walikuwa na nafas.Alikuwa mtu muhimu katika ile familia ambaye
angeweza kuwapa ujumbe ule, lakini aliamua kuudharau ujumbe ule na sasa
alikuwa akihofia juu ya watoto wake na mke wake.
Mateso yaliendelea pale ambapo mapepo yalipo mkata mikono
yake, aliangukia kwenye matope ya moto. Kwasababu ya maumivu toka tope lile
la moto, alijongea kama vile minyoo toka eneo moja hadi jingine. Nyama
zilimtoka mwilini mwake sababu ya ule moto. Alianza baadaye kutambaa kama
nyoka ili atoke pale. Lakini kila mara alipojaribu kwenda, mapepo
yalimsukuma na kumrudisha pale na alizama zaidi kwenye lile tope.
Baadaye tuliona idadi ya mapepo eneo moja.Kitu fulani
kilinivuta kuangalia, niliona kuwa mojawapo ya mapepo lilikuwa halina bawa
lake moja. Nilimuuliza Bwana, "Bwana, kwanini pepo hili halina bawa moja?"
Bwana alisema, "Pepo lile lilitumwa duniani kwa
lengo moja, lakini halikukamilisha kazi yake, na lilikemewa na mmoja wapo wa
watumishi wa Mungu na kurudishwa kuzimu. Baadaye Shetani alikuja na
kuliadhibu, na kulikata moja ya mabawa yake." Ndipo tulipo
gundua kuwa kama wakristo, tuna mamlaka ya kukemea mapepo yote na mamlaka
zote.
Mpendwa rafiki unaye sikiliza maneno haya sasa hivi, ushuhuda
huu sii kwa ajili ya kukuhukumu bali kwa wokovu; hivyo unaweza kujipima
mwenyewe na kuona hali ya roho yako mbele za Bwana. Hii ndivyo ilivyo ili
uweze kubadili njia zako kwa wokovu na sio kwa hukumu. Sasa hivi inua moyo
wako kwa Bwana na utubu dhambi zako, ili kama Bwana akija sasa hivi uweze
kwenda naye badala ya kwenda eneo lile la mateso mahali penye kilio na
kusaga meno. Hapa utajua ni kwanini Yesu alilipa gharama kubwa vile pale
msalabani Kalvari.
Tuliona watu wengi kuzimu ambao hawakujua ni kwa nini
walikuwepo pale. Maisha yao yalijaa mambo ambayo hawakuwahi kujua kuwa ni
dhambi. Mpendwa rafiki yangu, jipime mwenyewe! usifikiri kuwa kudanganya,
kuiba, maringo ni vitu sahihi vya kufanya! vyote hivi ni dhambi mbe;le za
macho ya Bwana! Mpendwa kaka, jeuka na acha kufanya vitu hivi!Ninakupa
ujumbe huu ili uache kufanya dhambi kwa kudhamiria, na kuuangalia zaidi uso
wa Bwana.
--- (Ushuhuda wa 6) ---
Zaburi 62:12 "Na fadhili ziko kwako, Ee Bwana;
maana ndiwe umlipaye kila mtu sawasawa na haki yake."
Asubuhi Bwana alitutembelea pale chumbani, alitushika mkono
na tulianza kwenda chini.Roho yangu ilikuwa imejawa na hofu, siwezi hata
kuielezea.Nilifahamu tuu kuwa siwezi kuuachia mkono wa mwokozi
wangu.Nilijisikia kuwa Yesu ni maisha yangu , mwanga wangu na kila tumaini
langu lilikuwa kwake; kama sivyo ningebakia mle kuzimu.Sikuwahi kuwaza kama
ningewahi kwenda eneo lile.Sikuamini pia kama eneo kama hili lipo.Japo ni
Mkristo nilifikiria kuwa kuna eneo linaloitwa Pagatori na labda ndilo kuzimu,
lakini Mungu alinionyesha ukweli wa Kuzimu.
Tulipofika kuzimu,nilijisikia mshituko wa eneo lile.Na mapepo
yote pale yalikimbia kujificha, kwasababu hakuna hata mojawapo ya pepo
linalo weza kusimama mbele ya uwepo wa Yesu..Tulisikia roho zilizo kamatwa
kuzimu zikipiga makelele ya nguvu, kwasababu walijua kuwa Yesu wa Nazarethi
yupo pale. Walijua wote kuwa yupo mtu mmoja tuu anaye weza kuwatoa eneo lile.
Walikuwa na matumaini hayo, japo ni matumaini ya uongo.
Tulitembea tukiwa tumeshikana mikono na Yesu, na tulifika
eneo la uzinzi. Yesu aligeuka kumwangalia mwanamke ambaye alikuwa amefunikwa
kabisa na moto. Wakati Yesu alipo mwona, alianza kutoka mle motoni taratibu,
japo maumivu yake hayakusimama.Tuliweza kuona kuwa alikuwa yuu uchi kabisa
na kuweza kuona mwili wake mzima. Mwili wake ulikuwa mchafu sana, na alikuwa
ananuka.. Nywele zake zilikuwa zimevurugika sana na alikuwa na tope la rangi
ya njano na kijani juu yake.Hakuwa na macho na midomo yake ilikuwa
imechanika. Hakuwa na masikio, ni machimo tuu. Kwa mikono yake, iliyo mifupa
iliyo geuka kuwa mweusi kwa moto, aliichukua ile nyama iliyo kuwa
inadondoka toka usoni mwake, na kujaribu kuirudishia. Lakini jambo hili
lilimpa maumivu mabaya zaidi.
Alitetemeka na kulia zaidi; kilio chake hakikukoma.Alikuwa
amejaa minyoo, na alikuwepo joka kubwa lililo jivingirisha mkononi mwake.
Lilikuwa ni nene sana na lenye miiba mwili mzima.Mwanamke huyu alikuwa na
alama ya namba 666 iliyo chimbiwa mwilini mwake;
namba ya mnyama iliyo tajwa katika kitabu cha Ufunuo. (Ufunuo
4:9-11) Alikuwa pia amevaa bango la chuma kifuani mwake, iliyo
tengenezwa na madini yasiyo fahamika, haikuwa inaweza kuteketezwa na moto..
Juu ya bango lile iliandikwa jambo fulani kwa lugha ngeni, lakini tuliweza
kuielewa.Ilisomeka, "Nipo hapa kwa ajili ya uzinzi."
Yesu alipo mwona alimuuliza, "Elena,
kwanini upo eneo hili?" Wakati akijibu, Elena alikuwa
akijipinda kutokana na maumivu yake. Alisema kuwa yupo pale kutokana na
uzinzi.Alimwomba Bwana msamaha tena na tena
Baadaye tulianza kuona tukio la kifo chake.Alipo kufa alikuwa
akifanya mapenzi na mmoja wa wapenzi wake, kwa sababu alifikiri kuwa
mwanamke aliye kuwa anaishi naye alikuwa amesafiri.Hata hivyo mwanaume yule
alirudi toka kazini na alimkuta akiwa kitandani pamoja na mwanaume
mwingine,Mwanaume yule alikwenda jikoni na kuchukua kisu kikubwa na alimpiga
nacho Elena nyuma mgongoni mwake.Elena alikufa na alichukuliwa kuzimu,
vilevile kama alivyo kufa; bado yupo uchi kabisa.
Kule kuzimu kila kitu kinaendelea, na bado anacho kile kisu
mgongoni mwake, kikimsababishia maumivu makubwa.Wakati huu alikuwa tayari
yupo kuzimu kwa miaka 7 na aliweza kukumbuka kila tukio la maisha yake na
kifo chake.Aliweza hata kukumbuka wakati mtu fulani alipo mhubiria habari za
Yesu; kwamba ndiye pekee anaye weza kumwokoa. Lakini sasa ilikuwa tayari
amechelewa sana na kwa kila aliyepo kuzimu.
Neno la Bwana linazungumza sana juu ya uzinzi, na lipo wazi
sana. Uzinzi ni kuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa.
1 Wakorintho 6:13 "Vyakula ni kwa tumbo, na
tumbo ni kwa vyakula;lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na
vyakula. Lakini mwili sii kwa zinaa, bali ni kwa Bwana naye Bwana ni kwa
mwili." pia katika
1 Wakorintho 6:18 "FIkimbieni
zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake mwewnyewe,
lakini yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe."
Wakati Yesu alipo maliza kuzungumza naye, alifunikwa na
blanketi kubwa la moto na hatukumwona tena. Lakini tulisika sauti ya mwili
wake ukiungua na makelele yale ya kutisha, siwezi hata kuyaelezea vizuri kwa
maneno.
Kwa jinsi tulivyo kuwa tunaendelea kutembea na Bwana,
alituonyesha watu wote pale: waabudu sanamu, wale wanao tumia na kufanya
uchawi,wasio safi,washerati, waongo, na wafiraji. Tuliogopa sana, kitu
pekee tulicho taka kufanya ni kuondoka pale.Lakini Yesu aliendelea kusema
kuwa ni muhimu kuendelea kuangalia ili tuwaeleze wengine, ili waweze kuamini.
Tuliendelea na Yesu na tulimshika mkono wake kwa nguvu
zaidi.Tlifika eneo ambalo lilinishangaza.Tulimwona kijana mdogo , wa miaka
23, akiwa ameinuliwa juu katikati ya moto. Hatukuweza kuona vizuri mateso
yake ni yapi, lakini ile namba 666 ilikuwa imechimbiwa mwilini mwake.
Alikuwa pia na bango lile kifuani mwake lililosomeka,"Nipo hapa kwa kuwa
wa kawaida." Alipo mwona Yesu, aliunyoosha mkono wake kwa Yesu akiomba
rehema. Neno la Mungu linasema katika
Mithali 14:12 "Iko njia ionekanayo kuwa sawa
machoni pa mtu, lakini mwisho wake ni njia za mauti."
Tuliposoma lile bango lililo sema, "Nipo hapa kwa kuwa wa
kawaida", Tulimuuliza Bwana"Bwana, inawezekanaje!? Inawezekana mtu
akaja eneo hili kwa sababu hii?" Ndipo Yesu akamuuliza, "Andrea,kwa
nini upo eneo hili?" Alijibu, "Yesu, nilipo kuwepo
duniani, nilifikiri kuwa , kuua, kuiba zilikuwa ndizo dhambi tuu, na ndiyo
sababu sikuwahi kujaribu kuja karibu yako." Katika
Zaburi 9:17 inasema "Wadhalimu watarejea kuzimu,
naam mataifa yote wanao msahau Mungu."
Andrea alifanya kosa kubwa kwa kugawa dhambi, kama wengi wa
watu wanavyo fanya leo.Bibilia ipo wazi sana inaposema mshahara wa dhambi ni
mauti , lakini karama ya Mungu ni uzima wa milele.(Warumi
6:23) Zaidi, wakati Bibilia inapo zungumza habari za dhambi, haigawi
dhambi, kwa sababu zote ni dhambi tuu. Andrea alikuwa na nafasi ya kumjua na
kumpokea Yesu, lakini hakuichukua nafasi ile ambayo Mungu alikuwa amempa.
Labda alikuwa na nafasi elfu kumjua Bwana, lakini hakutaka kumjua na hii
ndiyo sababu alikuwa pale. Baadaye blanketi kubwa la moto lilimfunika na
hatukumwona tena.
Tuliendelea
kutembea na Yesu. Kwa mbali tuliona kitu fulani kikidondoka kama maumbo
fulani hivi.Tulipo sogea karibu, tuliona kuwa ni watu wapya waliokuwa
wakiingia kuzimu muda ule.Watu ambao ndio tuu wakekufa duniani kabla
hawajampokea Yesu miyoyoni mwao, walikuwa wakiingia kuzimu.
Tulimwona kijana mmoja, mapepo mengi yalimkimbilia na kuanza
kuuharibu mwili wake. Mara mwili wake ulianza kujawa na minyoo. Alipiga
kelele, "Hapana! Ni nini hii? Acha! Sitaki kuwa eneo hili! Simamisha
hii! Hii lazima itakuwa ni ndoto!" Hakujua kuwa amekufa, na ya kuwa
amekufa bila ya Yesu moyoni mwake.Mapepo yalikuwa yakimchezea na kuuharibu
mwili wake. Baadaye namba 666 ilitokea kwenye upaji wa uso wake, na bango la
chuma kifuani mwake.Japo hatu kuweza kuona sababu ya yeye kuja kuzimu lakini
tulijua kuwa hataweza tena kutoka mle.
Bwana alituambia kuwa , mateso ya wote walio kuzimu yatakuwa
makubwa zaidi siku ya hukumu.Kama wanateseka kwa jinsi ile ya kutisha na ya
kuogopesha sasa, siwezi kufikiria jinsi gani watateseka siku ile ya hukumu.
Hatukumwona mtoto yeyote pale.Tuli waona vijana maelfu kwa
maelfu; wanaume kwa wanawake wa mataifa mengi. Hata hivyo kuzimu hakuna
utaifa au tabaka, wote wanakuja hapa kuteswa na kuhadhibiwa. Kuna kitu
kimoja ambacho kila mtu pale alikihitaji, na hicho ni nafasi tuu ya kutoka
mle ndani, angalau kwa sekunde. Wanataka pia kupata angalau tone la maji
kuuburudisha ndimi zao., kama vile habari ile ya tajiri kwenye Bibilia. (Luka
16:19) Lakini hii hili haliwezekani tena kwao, walikwisha chagua ni
wapi watakapo kaa milele. Walichagua umilele bila ya Mungu.Mungu kamwe
hampeleki mtu yeyote kuzimu, kila mmoja huenda kuzimu kutokana na matendo
yake mwenyewe katika
Wagalatia 6:7 "Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi;
kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakacho vuna."
Leo una nafasi kubwa ya kubadilisha mahali pako pa
umilele.Yesu bado anapatikana sasa, na Bibilia inasema kuwa wakati tukiwa
hai bado tuna matumaini.Leo una uhai, usikose nafasi hii, inaweza ikawa ni
ya mwisho kwako.
Mungu akubariki.
|